WABUNGE CCM MWANZA WASEMA MITANO TENA KWA MAGUFULI, WASIFU MAENDELEO YALIYOPATIKANA | Tarimo Blog

Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Mwanza
WABUNGE wa majimbo mbalimbali katika Mkoa Mwanza wamewaomba maelfu ya wananchi wa mkoa huo na Watanzania katika uchaguzi mkuu mwaka huu unaokwenda kufanyika Oktoba 28 kuhakikisha kura zote za urais zinakwenda kwa Dk.John Magufuli.

Wakizungumza leo Septemba 7,2020 katika Uwanja wa CCM jijini Mwanza kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea urais wa CCM Dk.Magufuli wabunge hao wamesema kazi kubwa iliyofanywa na Rais Magufuli kuna kila sababu ya kuoneshwa heshima kwa kupewa kura nyingi ambazo zinakwenda kuandika historia.

Wabunge hao wametaja hatua kwa hatua maendeleo ambayo yamefanyika katika majimbo yao yaliyoko ndani ya mkoa huo, lakini pamoja na maendeleo ambayo yamefanyika maeneo mbalimbali nchini na kuifanya nchi yetu kupiga hatua kubwa.

Mgombea ubunge wa jimbo la Kwimba mkoani Mwanza Shanif Mansoor amesema katika jimbo lao kabla ya Dk.Magufuli kuingia madarakani kulikuwa na changamoto nyingi na hasa ya uhaba wa maji.

Pia amesema yamefanyika mambo makuwa katika elimu, afya, barabara, miundombinu ya umeme, ujenzi wa mabweni, hospitali na aina nyingine ya miradi ya maendeleo imefanyika jimboni.

Kwa upande wake mgombea ubunge jimbo la Nyamagana amesema katika uchaguzi mkuu mwaka huu wanakila sababu ya kmchague tena Rais Magufuli kwani yote ambayo aliahidi katika jimbo hilo ametekeleza na wananchi wa Jiji la Mwanza na hasa Nyamagana ni mashahidi wa maendeleo makubwa yaliyofanyika.

“Nyamagana tumepiga hatua sana ya kimaendeleo, Rais Magufuli aliahidi kujenga madaraja na yote amejenga, aliahidi kutujengea barabara na kazi hiyo ameifanya , tulikuwa na kilometa tisa za vumbi katikati ya jiji lakini zote sasa zimejengwa kwa lami,”amesema Mabula.

Pia amesema Nyamagana ina kila aina ya wafanyabiashar lakini katika kuweka mazingira mazuri, Rais Magufuli ameweka utaratibu mzuri na leo wafanyabiashara wako huru kufanya biashara zao na hakuna anayewasumbua.

Wakati huo huo mgombea ubunge jimbo la Buchosa Erick Shigongo kabla ya kumuombea kura mgombea urais wa CCM Dk.Magufuli, amesema “Nimesimama mbele yenu kusimama kusema jambo.

“Mtu yoyote anaweza kuwa kitu chochote, baba yangu alishiriki ujenzi wa uwanja huu (CCM Kirumba) lakini leo nimesimama mbele ya uwanja huu kuomba kura.

“Hata ninyi mnaweza kukaa mbele.Nawaomba Oktoba 28 mwaka huu Watanzania wote tukamchague mgombea urais wa CCM Dk.John Magufuli,yaliyofanyika mwenye macho haambiwi Tanzania tazama na Tanzania inaendelea kujengwa,”amesema.

Ameongeza Dk.Magufuli ni mtu mwaminifu, mtu mwadilifu ni mtu anayeaminika , anapenda na kujali wanyonge, ni mtu wa vitendo sio maneno wala porojo , hivyo oktoba 28 iwe siku ya kumchague ili aongeze tena nchi yetu kwa miaka mitano.

Shigongo amesema kupitia Rais Magufuli, nchi yetu hivi sasa imefikia uchumi wa kati , hivyo hakuna sababu ya Watanzania makosa hata kidogo.”Tunataka kuvunja rekodi kwa kumpa kura .

“Wananchi wa jimbo la Buchosa ambao manisikiliza muda huu,mmeniamini, mmenituma nikawe mtumwa, nimekubali kuwa mtumwa wenu, nitumeni.Nitawatumikia kwa uaminifu mkubwa, na chini ya Rais Dk.Magufuli nchi yetu inakwenda mbele,”amesema Shigongo

Wakati huo huo mgombea ubunge wa jimbo la Magu Boniveture Kiswaga amesema kura hukomesha mashindano , hivyo oktoba 28 mwaka huu wanakwenda kumaliza ubishi kwa kumchagua Dk.Magufuli.

“Rais Magufuli ambaye leo anarudi tena kw Watanzania kuomba ridhaa ya kuongoza nchi kwa miaka mingine mitano amefanya mengi, ameitendea haki Tanzania, kura nyingi katika uchaguzi wa mwaka huu ziende kwa Magufuli,”amesema.

Kwa upande wake Alezander Mnyeti ambaye yeye amepita bila kupingwa jimbo la Misungwi ametumia nafasi hiyo kumuombea kura Dk.Magufuli akawe Rais kwa miaka mingine mitano.

“Kule Misungwi kwenye nafasi ya ubunge na madiwani tumeshamaliza kazi, hivyo kwa sasa tunasubiri Oktoba 28 mwaka huu tukamalize kazi kwa kumpitisha Dk.Magufuli,”amesema Mnyeti.

Mgombea ubunge jimbo la Ilemela ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ametumia nafasi hiyo kuelezea utekelezaji wa Ilani katika katika kutatua changamoto za migogoro ya ardhi iliyokuwepo na chini ya Rais Magufuli kwa sasaa wamefanikiwa kukomesha migogoro hiy na hali iko shwari.

Kuhusu jimbo la Ilemela Mabula amesema kuna maendeleo makubwa yamefanyika katika sekta mbalimbali za afya, elimu, maji, barabara elimu bure, umeme pamoja na kuboresha maisha ya watu kwa kuweka mazingira mazuri ya kufanya shughuli zao za kila siku.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2