WANANCHI MWANZA WANA JAMBO LAO...DK. MAGUFULI AWAAMBIA KUONGOZA NI MSALABA,AMEJITOA SADAKA | Tarimo Blog

Wananchi wa jiji la Mwanza wakiwa wamejitokeza kwa wingi katika maeneo ya Igoma, Nyakato Buzuluga na Mabatini jijini Mwanza kumpokea Mgombea wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ambaye amewasili mkoani Mwanza kwa ajili ya Mkutano wa Kampeni za Urais hapo kesho ktk uwanja wa CCM Kirumba.


Na Said Mwishehe, Michuzi TV- Mwanza


MGOMBEA Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dk.John Magufuli amewaeleza wananchi wa maeneo mbalimbali kuanzia Magu na kisha Igoma, Nyakato,Mabatini ,Nyamagana na Kisesa kwamba kuongoza ni msalaba na sadaka na inahitaji moyo kwani licha ya kuleta maendeleo bado wapo wanaoendelea kutukana lakini yeye ameamua kuwatumikia Watanzania ili aendelee kuleta maendeleo.

Amewahakikishia wananchi hao kuwa anawapenda na kwa mapokezi ambayo wamemuoonesha alipokuwa akiingia Jiji la Mwanza atabaki na deni na atalilipa kwa kuwaletea maendeleo zaidi ya yaliyopatikana katika kipindi cha miaka mitano ya uongozi wake na Chama chake cha CCM.

"Mwaka 2015 hakukua hivi lakini baada ya kuingia madarakani tulianza kazi ya kuleta maendeleo na tutaendelea na kazi hiyo kwasababu tunaiweza na ndio maana tumekuja tena kwenu kuomba mtuchagua CCM tukafanye kazi,"amesema.

Hata hivyo ameleeza Mwanza kwa sasa wilaya mbili,hivyo kwa mawazo yake ataongeza wilaya nyingine ya tatu iwapo atachaguliwa huku akifafanua kwamba kutakapakuwa na wilaya nyingine na bajeti itaongezeka,hivyo kuongeza kasi ya ukuaji wa maendeleo.

Akizungumza na wananchi hao ameeleza pamoja na mafanikio zipo baadhi ya changamoto na anazifahamu ikiwemo changamoto ya maji na kwamba tayari mkandarasi ameshasaini mkataba na tatizo la uhaba wa maji linakwenda kumalizika.

Hata hivyo ameendelea kuwaomba wananchi wa mkoa wa Mwanza huo kumpa kura ili kuwaoneesha wale ambao wamekuwa na kazi ya kupinga maendeleo na kwamba Tanzania imetoka mbali,iko mbali na inakwenda mbali.

Dk.Magufuli akiwa eneo la Mabatini amewashukuru wananchi kwa makaribisho mazuri ambayo wamemuonesha.Maelfu walikuwa wamekusanyika eneo la darajani ."Nawaomba Oktoba 28 mkanipigie kura mimi , wabunge na madiwani.





Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2