WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AFUNGUA MBIO ZA NMB MARATHON NA KUTOA ZAWADI KWA WASHINDI | Tarimo Blog


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi pamoja na washindi wa Mbio za  NMB Marathon  baada ya kuwakabidhi zawadi washindi hao kwenye viwanja vya Mlimani City jijini Dar es salaam, Septemba 12, 2020. Wa nne kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji, Angellah Kairuki , wa tatu kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Abubakar Kunenge, Wa pili kulia   ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna  na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji, Hospitali ya Taifa Muhimbili,  Profesa Lawrence Maseru. Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Sanlam East Africa, Julius Magabe na wa tatu kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NMB, Dkt. Edwin Mhede.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,  Uwekezaji, Angellah Kairuki wakati alipowasili kwenye  viwanja vya Mlimani City jijini Dar es salaam kufungua Mbio za NMB Marathon  na kutoa zawadi kwa washindi Septemba 12, 2020.  Wa pili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Abubakar Kunenge na kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NMB,  Dkt. Edwin Mhede.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi hundi ya sh. Milioni 100 Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Profesa Lawrence Maseru, (kushoto) wakati alipohitimisha  Mbio za NMB Marathon kwenye viwanja vya Mlimani City jijini Dar es salaam, Septemba 12, 2020. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Uwekezaji) Angellah Kairuki, wa tatu kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna, wa pili kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Sanlam  East Africa, Julius Magabe na wa tatu kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NMB, Dkt.Edwin Mhede. Fedha hizo zilizotolewa na Benki ya NMB zitatumika kuwasaidia watoto wenye ugonjwa saratani wanaotibiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2