Baadhi ya washiriki waliohudhuria mkutano huo.
*Atoa neno kwa JPM
Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
IMEELEZWA kuwa Rais Magufuli hawezi kutenganishwa na maslahi ya Taifa wala kutenganishwa na juhudi zake za kupingana na rushwa, ufisadi na pamoja na ujenzi wa miundombinu imara ya usafiri iliyoipeleka taifa katika uchumi wa kati.
Hayo yameelezwa leo na mwangalizi mkuu wa kimataifa na kimataifa ya Wapo Mission International, Askofu Sylvester Gamanywa wakati akizindua kitabu chake cha "Uzalendo na Falsafa ya Mamlaka" jijini Dar es Salaam.
Gamwanywa amesema kuwa kitabu hicho chenye sura sita kina mlengo wa kutoa elimu ya uraia kwa wananchi.
"Kitabu hiki kitatufaa hata baada ya uchaguzi, na kikisomwa na wagombea na wananchi kwa siku 20 zilizobaki katika kuelekea uchaguzi mkuu mitazamo yao itabadilika...kimeeleza na kuhamasisha wananchi kujua aina ya kura watakazopiga aidha za Uzalendo au usaliti" ameeleza Gamanywa.
Askofu Gamanywa amesema, watumishi wa Mungu hawawezi kumtenganisha Rais Magufuli na Uhuru wa ibada;
"Kama si Rais Magufuli tungekuwa hatuhubiri Injili na kuendesha ibada, Kama si Rais Magufuli Corona ingetumaliza kwa sababu hatukuwa na uwezo kudhibiti kisayansi na hadi sasa wanasayansi wameshindwa kudhibiti" amesema.
Aidha amesema kuwa uzalendo wa nchi ni kumwongezea Rais Magufuli kipindi cha pili ili andeleze mikakati ya kiuchumi kutoka uchumi wa kati kwenda uchumi wa kwanza.
"Kuna watu wanasema natumika huku mara kule..ninasema ukweli ninaoujua na uliokuwa hausemwi ili hata nikienda kwenye kiti cha hukumu nimwambie Mungu kuwa nilisema ukweli, kumwondoa Rais Magufuli kwa Sasa ili asiweze kukamilisha miradi mikubwa ya kiuchumi aliyoiasisi na kumwondoa kwenye udhibiti wa rasilimali za nchi ni sawa na kuirudisha Tanzania kwenye umaskini na kuiuza nchi kwa mabeberu na huu ndio usaliti dhidi ya nchi." ameeleza Gwamanywa.
Aidha amesema kuwa wanasiasa lazima wawe wazalendo kwa kuepuka masuala ya ukabila, udini na majimbo mambo ambayo yanaweza kuigawa nchi.
Kwa upande wake Sheikh. Mohamed Iddi Mohamed amesema viongozi wa dini ni watu wa kushirikisha elimu kwa Umma ni si kuikosoa Serikali.
"Nimeandika vitabu viwili ambavyo vikisomwa mitazamo ya jamii yetu itabadilika hasa kwa wakati huu...nimeandika kitabu cha Nasaha kumi kuelekea uchaguzi mkuu na misingi 15 ya amani na lazima tushirikiane kutunza tunu za taifa" ameeleza.
Sheikh. Mohamed amesema watanzania lazima wachague kiongozi mzalendo, mwenye kujitoa kwa nchi na mwenye maono chanya kwa taifa.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment