WIZARA YA FEDHA KUIMARIKA KIELETRONIKI | Tarimo Blog

 
Na Epifania Gustafu -MAELEZO

SERIKALI imewaagiza maafisa masuhuli wote wa taasisi zilizo chini ya Ofisi
ya Msajili wa Hazina kuhakikisha kuwa mpango wa bajeti kwa mwaka
2021/2022 unaandaliwa kwa mfumo mpya wa uandaji wa bajeti,
(PlanRep.)

Akizungumza katika uzinduzi wa mfumo wa uandaaji wa bajeti jijini
Dodoma, Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Mary Maganga,
amemtaka Msajili wa Hazina Athumani Mbutuka kutochambua bajeti
yoyote itakayowasilishwa nje ya mfumo huo.

Pia amempongeza Msajili huyo kwa utekelezaji wa mfumo huo ambao ni
matokeo ya juhudi zilizofanywa na ofisi yake katika kuimarisha usimamizi
wa fedha za umma katika Wakala za Serikali.

Aidha amewashukuru wadau wa maendeleo wanaofadhili Mradi wa
Maboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (PFMRP) kwa kuwezesha
kifedha ujengaji wa mfumo huo na kuendelea kufanya kazi kwa
kushirikiana na Serikali katika kuimarisha nchi.

"Nawapongeza kwa dhati vijana wetu, Watanzania wenzetu, ndani ya
Serikali kwa weledi wao na jitihada zao zilizosababisha kufanikisha
kujenga customization ya mfumo huu, hongereni sana hatuna budi
kuishukuru Serikali ya Awamu ya Tano , kwani mafanikio yote haya
yamewezekana chini ya uongozi wake thabiti na imara." Amesema
Maganga.

Ameongeza kuwa uwepo wa mfumo huo utapunguza upotevu wa mapato,
kuimarisha na kuchochea uwajibikaji, kuimarisha uchambuzi wa bajeti na
ufuatiliaji na hatimaye kuongeza mapato katika mfuko Mkuu wa Serikali.
"Nafahamu ofisi yako haikuwa na mfumo ambao ungeiwezesha kufualitia
utekelezaji wa bajeti za Wakala wa Serikali, Taasisi na Mashirika ya
Umma, Hivyo basi, mfumo huu utakuwa kitendea kazi muhimu cha ofisi
yako na naamini hata Wizara na Taasisi nyingne za Serikali kuu zitaweza
kutumia mfumo na kuweza kuokoa gharama ambazo zinalipwa kwa ajili ya
mfumo wa kibajeti." Amesema Maganga.

Amebainisha kuwa mfumo huo utaunganishwa na mfumo wa ulipaji
Serikalini (MUSE) na kuwezesha kudhibiti matumizi ya fedha za umma
nje ya mipango na bajeti iliyoidhinishwa.

Kwa upande wa Msajili wa Hazina, Athumani Mbutuka amesema Ofisi hiyo
ikishirikiana na Ofisi ya Rais, TAMISEMI na Wizara ya Fedha na Mipango
katika mwaka wa Fedha 20219/20 ilianzisha mradi wa kusimika Mfumo wa
uandaaji na uwasilishaji wa bajeti Kielectronik (PlanRep) utakaotumika
katika Wakala za Serikali,Taasisi na Mashirika ya Umma.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2