RAIS wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt.John Magufuli na Rais wa Malawi, Lazarus Chakwera wakipeana mikono mara baada ya kuzindua kituo cha mabasi mikoa mbali mbali na nchi za jirani jijini Dar es Salaam leo Oktoba8,2020.
*RAIS WA TANZANIA NA RAIS WA MALAWI WAWEKA JIWE LA MSINGI KITUO CHA MABASI MBEZI
Na Lusajo Frank DSJ
RAIS wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli na Rais wa Malawi Lazarus Chakwera wameweka jiwe la msingi katika kituo kipya cha mabasi Mbezi kinachotarajiwa kukamilika mwezi January mwakani.
Awali kituo hicho kilitarajiwa kumalizika mwezi wa saba lakini kutokana janga la Corona kulikumba ulimwengu, imeathiri mradi huo kutomalizika kwa wakati uliopangwa.
Rais Dkt.Magufuli ametoa maagizo, kwa waziri wa wizara husika kumkata Pesa mkandarasi kwa kuchelewesha mradi na kutoa nasaha kwa wakandarasi kuacha kutafuta kisingio cha Corona, kwani Tanzania tupo salama na hakuna Corona.
"Tukienda kwa utaratibu huu, miradi mingi itachelewa na mimi nimeumbwa kusema ukweli kwa sababu msema kweli ni mpenzi wa Mungu na ninazungumza mbele ya baba Askofu mstaafu, Dr. Lazarus Chakwera." Amesema Rais Dkt.Magufuli.
Kituo hicho kinatarajiwa kuwa na uwezo wa kubeba mabasi 1,000 na teksi 280 kwa siku, Pia kutakuwa na maeneo ya bodaboda na bajaji na na eneo la mamalishe na babalishe.
Mradi huo umegharimu kiasi cha dola za kimarekani milioni 22 utasaidia kupunguza msongamano wa mabasi yaendayo mikoani kwa kiasi kikubwa hadi sasa mradi huo umefikia asilimia 80.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment