KATIBU UWT DODOMA MJINI AWAOMBA WANAWAKE KUTOHADAIWA NA AHADI HEWA | Tarimo Blog

Charles James, Michuzi TV
MSIHADAIKE! Hiyo ndio kauli ya Katibu wa Umoja wa Wanawake wa CCM Wilaya ya Dodoma Mjini, Diana Madukwa akiwaeleza akina mama wa Wilaya hiyo kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba 28, mwaka huu.

Madukwa ameitoa kauli hiyo alipokua kwenye vikao vya ndani na wanawake wa Wilaya ya Dodoma Mjini ambapo anapita kutafuta kura za kishindo kwa Mgombea Urais wa CCM, Dk John Magufuli, Mgombea Ubunge Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde na madiwani.

Akizungumza na wanawake wa UWT kata za Mpunguzi, Mbabala na Nala amesema miaka mitano ya Dk Magufuli imekua ya heshima sana kwa Dodoma kwani licha ya kuihamishia serikali hapa lakini pia kitendo cha kuipa Dodoma hadhi ya Jiji kumeongeza fursa kubwa za kimaendeleo.

Amesema miaka mitano ya Dk Magufuli imeshuhudia Jiji hilo likiongoza kwa mapato, likiongoza kwa mtandao wa lami nchini kwa kuwa na Km 129 pamoja na kuletewa miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo Stendi ya kisasa, Soko kubwa Afrika Mashariki pamoja na eneo la mapumziko la Chinangali.

" Niwaombe akina Mama msihadaike na wapinzani, nimepata taarifa wanapita kwenu kuwalaghai muwape vitambulisho vya kupigia kura, msijaribu kufanya hivyo kwani mtapoteza haki yenu ya msingi, msidanganywe na maneno yenu hawana uwezo wa kuongoza kwa sababu vyama vyao wenyewe tu vinawashinda, mambo yaliyofanywa na Dk Magufuli kwa miaka mitano kiongozi mwingine angeyafanya kwa miaka 20, tusimuangushe twendeni tukampe kura nyingi za kishindo.

Wapinzani wanachohubiri wao ni maandamano tu, sasa ndugu zangu sisi tunataka kuandamana au tunataka maendeleo? Hawana hata ilani ya Uchaguzi, sisi tukija tunasema tumejenga vituo vya afya 480, tumejenga hositali ya Wilaya 71, tumekarabati shule kongwe, tumetoa elimu bure, wao wakija watasema nini? Tusihadaike Oktoba 28 tukamchague Magufuli," Amesema Madukwa.
Katibu wa UWT Wilaya ya Dodoma Mjini (mwenye tisheti ya Bendera ya Taifa) akiwa katika picha ya pamoja na akina Mama wa Kata ya Mbabala baada ya kumaliza kufanya nao kikao cha ndani cha kutafuta kura za Mgombea Urais wa CCM, Dk John Magufuli.
Katibu wa UWT Wilaya ya Dodoma Mjini, Diana Madukwa akizungumza na akina Mama wa Kata ya Mpunguzi (hawapo pichani) alipofanya nao mkutano wa ndani wa kutafuta kura za CCM Wilaya hiyo.
Wanawake wa UWT Wilaya ya Dodoma Mjini wakionesha picha za Mgombea Urais wa CCM, Dk John Magufuli ikiwa ni ishara ya kumchagua kwa kura za kishindo kwenye uchaguzi mkuu Oktoba 28.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2