Mbunge Mteule wa Jimbo la Bumbuli, January Makamba amewaomba watanzania wasicheze kamali katika kuchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania badala yake wampigie kura Rais Magufuli sababu ni mzalendo ,mcha Mungu na jasiri.
Ombi hilo amelitoa wakati wa ziara yake ya muendelezo wa kupita vijiji kwa vijiji kusaka kura za mgombea urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha mapinduzi CCM Dk Magufuli na Madiwani wa chama hicho.
Alisema kuwa Rais Magufuli ana maono ni mzoefu katika uongozi na anatoka kwenye chama ambacho kina ilani ,sera na mipango bora tofauti
na wagombea wengine ambao sifa zao ni uanarakati na hawana uzoefu wa kuongoza nchi wao binafsi na vyama vyao.
Makamba ambaye pia ni Katibu mstaafu wa Halmashauri kuu ya Taifa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI) aliwataka wananchi ifikapo October 28 wasihadaike kuchagua vyama vingine bali wamchague Magufuli ambaye ni mzoefu wa uongozi na anatoka kwenye chama chenye historia na uzoefu wa kuongoza nchi,bunge na halamshauri.
" Tunakubali kila mmoja anasifa zake lakini sifa ya kushika hatamu ya uongozi wa nchi na kuamrisha vyombo vya ulinzi na usalama vilinde amani , mipaka ya nchi na utulivu anayo Magufuli hivyo msicheze kamali wala msikengeuke kuchagua siku ya uchaguzi itakapofika"Alisema Makamba.
Alisisistiza kuwa CCM inarekodi ya maendeleo tofauti na vyama vingine
mfano sera ya elimu bure,mpango kufikisha umeme vijijini wa Rea ,maji vijijini ,vituo vya afya kila kata na zahanati kila kijiji na kwamba chama cha mapinduzi kimeviacha mbali vyama vingine ambavyo havipangi bajeti, havikusanyi kodi,havisukumi maendeleo wala havisimamii maendeleo.
Alisema CCM imefanya mengi ya kimaendeleo na imebadilisha maisha ya watanzania kwa ubora zaidi hivyo aliwataka wananchi wasiache Mbachao kwa msala upitao sababu CCM bado inadhamira ya dhati ya kuwatumikia na kuwaletea maendeleo ya haraka.
Alisema wagombea wa upinzani hawana sera na mipango nakwamba hata
kwenye mikutano yao hawazungumzii suala zima la kuletamaendeleo kwa wananchi bali ni matusi na kejeli .
" Nimepata kusikiliza hotuba ya Mgombea mmoja ivi wa Urais wa upinzani dakika 30 nzima, dakika 26 anazungumza kejeli ,matusi ,lawama mara mgombea wa CCM kafanya hivi kafanya vile ndani ya dakika zote hizo hakuzunguzia maji ,umeme,afya wala barabara wakati Magufuli ukimsikiliza hotuba zake anazungumzia mahitaji ya wananchi na mambo yanayowagusa moja kwa moja "alisema Makamba anayesubiria kuapishwa baada ya kupita bila kupingwa.
Hata hivyo Makamba amewaomba wananchi waiamini tena CCM kwa kumchagua Rais Magufuli kutokana na jitihada alizofanya katika kipindi cha miaka mitano iliopita cha kudhibiti wizi ,rushwa na ufisadi serikalini pamoja nakulinda rasilimali za nchi.
Alisema kuwa Mgombea wa CCM ambaye anamaliza kipindi chake cha awamu ya kwanza ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani licha ya kufanya mambo mengi ya kimaendeleo lakini pia amefanikiwa pia kurudisha nidhamu katika utumishi wa umma na kurudisha chachu mpya ya Watanzania ya kujitafutia Maendeleo.
" Naomba ndugu zangu muendelee kutuamini sisi CCM ili tuendelee kuwa tumikia kupunguza changamoto zilizobakia pamoja na kuendelea kukamata Ikulu ,Bunge na Halmashauri ya Bumbuli"alisema January Makamba ambaye kwa sasa ni Mbunge Mteule Wa Jimbo la Bumbuli.
Alisema kwa mujibu wa katiba ya nchi na utamaduni mamlaka ya kuchagua yapo kwa wananchi na ndio maana kila baada ya miaka mitano inatengenezwa ratiba ya vyama vyote kuja kuomba fursa na heshima ili kuomba ridhaa ya kuwatumikia tena katika kipindi kijacho.
Makamba alisisistiza vyama vya upinzani haviwezi kupewa nchi sababu havijakomaa labda huko mbeleeni vikikomaa vinaweza kupewa nchi kwani labda.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment