Na Mwandishi wetu, Hanang`
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Hanang' Mkoani Manyara kwa tiketi ya CCM,
mhandisi Samwel Hhayuma amewasilisha changamoto zinazoikabili Jimbo
hilo kwa mgombea mwenza wa urais kwa bendera ya CCM, Samia Suluhu Hassan.
Mhandisi Hhayuma ametoa changamoto hizo wakati akizungumza kwenye
mkutano wa kampeni uliofanyika katika Mji mdogo wa Katesh.
Hhayuma ametaja baadhi ya changamoto zinazowakabili wananchi wa jimbo hilo ni pamoja na ubovu wa miundombinu ya barabara, Maji na nishati ya umeme vijijini.
Ameeleza kuwa, wanaomba kujengewa kilomita 10 za barabara ya lami kwenye mji mdogo wa Katesh na lami kutoka kata ya Mogitu hadi hospitali ya Kilutheri ya Haydon Wilayani Mbulu.
Amesema changamoto za maji zinawakabili baadhi ya wananchi na hiyo ni kutokana kutokamilika mradi wa maji wa thamani ya sh. bilioni 2 wa kutoka
kata ya Mogitu hadi mji mdogo wa Katesh.
"Pia kuna changamoto ya nishati ya umeme kwani ni asilimia 75 pekee ya
vijiji vya jimbo la Hanang' ndiko kuna umeme bado asilimia 25 ya
vijiji ambavyo havina umeme," amesema mhandisi Hhayuma.
Hata hivyo, mgombea mwenza wa kiti cha Urais kupitia CCM Samia amesema kupitia ilani ya uchaguzi wa CCM changamoto nyingi zilizotajwa na mhandisi Hhayuma zitapatiwa ufumbuzi kwa kutekelezwa kwa mwaka 2020/2025.
Amesema miradi ya maji itakamilishwa, umeme utafika vijiji vyote na
barabara ya lami ya Mogitu hadi Haydom itajengwa kwani ipo kwenye
ilani ya uchaguzi kwa mwaka 2020/2025.
"Ili kukamilisha hayo tunaomba muichague CCM kwa kumpa kura nyingi
Rais John Magufuli, mhandisi Hhayuma na madiwani wanaotokana na CCM."
amesema Samia.
Waziri mkuu mstaafu Fredrick Sumaye amesema mhandisi Hhayuma ni kijana
msomi ambaye anaweza hata kuchaguliwa kuwa Waziri pindi akichaguliwa
kuwa mbunge na Rais Magufuli atakaposhinda tena.
Sumaye amesema wananchi wa Hanang' wasipotoshwe na wapinzani na
kupoteza kura zao kwani muda wa siasa umeshapita kimachotakiwa ni
maendeleo pekee.
Mbunge wa jimbo hilo wa kipindi kilichopita, Dkt. Mary Nagu alisema
mradi wa maji wa Mogitu hadi Katesh wa gharama ya sh2 bilioni
umechukua muda mrefu bila kukamilika.
"Maji ni uhai na inabidi mradi huu uelekezewe nguvu zaidi ili uweze
kukamilika na wananchi wa eneo hili la Katesh wapate maji ya
uhakikika," amesema Dkt. Nagu.
Mshindi wa ubunge wa jimbo hilo kupitia kura za maoni ya chama hicho,
George Bajuta amesema wanaosema amenuna baada ya jina lake kukatwa ni
waongo kwani anaunga mkono uamuzi wa CCM kwa asilimia 100.
"Baba yako akiamua mwingine akachunge ng'ombe hupaswi kulalamika kazi
zipo nyingi huenda nikatumwa kuuza duka au nikapewa kazi nyingine,"
ameeleza Bajuta.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment