OFISI ZA AZAKI ZAFUNGULIWA JIJINI DODOMA, 'SERIKALI IMEWEKA MAZINGIRA MAZURI KWETU' | Tarimo Blog

 


Charles James, Michuzi TV


Asasi za Kiraia hapa nchini (AZAKI) imezindua Ofisi yake pamoja na kituo jijini Dodoma hali itakayosaidia upatikanaji wa taarifa na maarifa muhimu kuhusu asasi hizo kwa wananchi na serikali kwa wakati.


Akizindua Ofisi hiyo Jijini Dodoma Msajili wa Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali  Vickness Mayao, amesema Mashirika hayo yamekuwa na mchango mkubwa katika kuleta maendeleo kwa wananchi na kusaidia kuondokana na umaskini.


Amesema Serikali inatambua mchango mkubwa unaofanywa na Asasi hizo na kuahidi kuwa serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa mashirika hayo  kufanya kazi zao na kuwa kiunganishi kati ya maendeleo na wananchi.


"Serikali imeweka mazingira mazuri na wezeshi kwa mashirika na asasi za Kiraia kufanya kazi na tumeweka miongozo itakayowezesha asasi na mashirika hayo kufanya kazi zao" amesema bi Vickness.


Amesema kuzinduliwa kwa kituo hicho ambacho ni makao makuu ya AZAKI kutasaidia kupatikana haraka kwa taarifa kwa wananchi  zinazohusu AZAKI kwa wahitaji ikiwamo serikali inayosimamia utendaji kazi wa mashirika au asasi hizo.


Aidha amezitaka Asasi hizo kufanya kazi kwa kufuata misingi inayoziongoza Asasi hizo kufanya kazi bila kukiuka misingi yake ikiwamo kufanya kazi kwa kushirikiana katika kuhudumia wananchi katika kuleta maendeleo.


Kwa upande wake raisi wa Asasi za kiraia hapa nchini Dkt Stigmata Tenga amesema tangu kuanza kufanya kazi kwa AZAKI hapa miaka 18 iliyopita hapa nchini wametoa ruzuku kwa mashirika elfu sita (6000) na kuziwezesha asasi elfu 10 katika kutekeleza majukumu yao hapa nchini.


Aidha amesema kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya upatikanaji wa taarifa na maarifa kuhusu  AZAKI wameamua kufungua ofisi ili taarifa zipatikane mapema kwa wadau wa AZAKI na wadau wengine kuhusu sekta ya asasi za kiraia.


" Uhitaji wa taarifa umeongezeka Sana mfano mwanafunzi wa UDOM akijakupata taarifa atapata hapa mtu akitaka kuanzisha shirika lazima aje hapa kufuata utaratibu kabla ya kuja serikalini kusajili shirika hilo" amesema Dkt Stigmata Tenga.


Amesema kufunguliwa kwa ofisi hiyo kutawezesha kwa kila mtu atakayepata nafasi ya kutembelea kituo hicho atakutana na wadau wengine wa Maendeleo na kupata taarifa, kujifunza na kukuza ushirikiano ndani ya sekta ya AZAKI.


Aidha amebainisha kuwa kupitia utoaji wa ruzuku na huduma za kujenga uwezo kwa AZAKI wamefanya nazo kazi wameweza kuwafikia wananchi zaidi ya milioni therathini na moja (mil. 31) kote hapa nchini ikijumuisha bara na visiwani.


Nae Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa Sekta kutoka TAMISEMI, Mhandisi Enock Nyanda amesema TAMISEMI wako hatua za mwisho kukamilisha ugatuaji kitaifa utakaowezesha kuendeleza uchumi wa maeneo ili kujenga uchumi wa maeneo kuhamasisha wananchi kujishughurisha kwa mambo mbali mbali yatakayowawezesha kujikwamua kiuchumi.


Kituo cha AZAKI Tanzania, hiki ni kituo cha taarifa na maarifa kwa wadau mbalimbali wa sekta ya AZAKI,asasi za kijamii, watunga sera, sekta binafsi, taasisi za kitaaluma na utafiti, maafisa wa Serikali, Jumuiya za kimataifa na wananchi kwa ujumla kwa ajili ya kupata taarifa zinazohusu AZAKI.

 Msajili wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO’S) Bi.Vickness Mayao,akitoa neno wakati wa uzinduzi wa Ofisi ndogo ya Foundation For Civil Society pamoja na Kituo cha Azaki jijini Dodoma.

 Msajili wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO’S) Vickness Mayao,akitoa neno wakati wa uzinduzi wa Ofisi ndogo ya Foundation For Civil Society pamoja na Kituo cha Azaki jijini Dodoma.

Msajili wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO’S), Vickness Mayao,akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa  Ofisi ndogo ya Foundation For Civil Society pamoja na Kituo cha Azaki hafla iliyofanyika jijini Dodoma


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2