SHULE YA SEKONDARI ST. METHEW'S KUANZISHA MASOMO YA USHONAJI NA UPISHI | Tarimo Blog

Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii

SHULE ya Sekondari St. Methew's mbioni kianzisha masomo ya upishi na ushonaji ikiwa na lengo la wanafunzi wanaohitimu masomo katika shule hiyo kuacha kuzurula kutafuta kazi au kipato.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mutembei Holding Limited (MHL), Peter Mutembei wakati akizungumza katika Mahafali ya 20 ya shule ya Sekondri St. Methew's iliyopo Mpakani mwa jiji la Dar es Salaam na mkoa wa Pwani, mahafali iliyofanyika mwishoni mwa wiki Oktoba 3, 2020. Alisema kuwa masomo hayo yanawasaidia katika shughuli za uzalishaji mali na ni njia bora ya kumuepusha na vishawishi kutoka makundi mabaya katika jamii.

Hata hivyo Mutembei alisema kuwa shule ya Sekondari St. Methew's imejikita zaidi katika malezi bora ya Mtoto ambayo yatamwezesha kujua hili ni baya na hili ni zuri la kufanya.

"Shuleni hapa tunawafunzisha uzalendo, maadili mema na nidhamu, ikiwa tunaushirikiano mwema na serikali ambapo wataalamu mbalimbali wameanza kufika shuleni kwetu kutoa mafunzo ya nidhamu."

Amesema katika kusimamia malezi, hawataki kuwajengea watoto nidhamu ya woga wakiwa na dhamira ya kumuandaa mtoto kujua hili ni baya hawezi kufanya hata kama hakuna mtu anamwona.

Kwa Upande Afisa elimu Mkoa wa Mkuranga, Hadija mcheka alisema kuwa wao kama Serikali wataendelea kudumisha ushirikiano uliopo na shule ya Sekondari St. Methew's ili kuleta matokeo chanya zaidi katika utoaji wa elimu.

"Tutahakikisha kwamba watoto wa Kitanzania wanapata elimu iliyobora katika mazingira bora, kama serikali tunaendelea kuboresha huduma ya elimu, tumeanza kufanya Ukarabati katika shule zetu, tunaendela kuajiri walimu pale ambapo kunakuaa na upungufu wa walimu...." Alisema Hadija

Hata hivyo Hadija Alisema kuwa lengo la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kuhakikisha kila mtoto anapata hakia ya elimu bila kuwa na kipingamizi chochote.

"Serikali imehakikisha kila mtoto anapata elimu, kwa yule anayeshindwa kwenda shule za Serikali ama mzazi amebarikiwa kipata basi Mlete mwanao kwa shule za Mutembei na huu ndio ushirikiano tulionao kati ya shule binafsi na Serikali...." Alisema Hadija

Afisa Elimu Mkoa wa Pwani,  Hadija Mcheka akipokea Sabuni zilizotengenezwa na wanafunzi aa shule ya Sekondari St. Methew's katika Mahafali ya 20 ya Shule hiyo yaliyofanyika Mwishoni mwa wiki Oktoba 3, 2020.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shule za Mutembei Holding Limited, Peter Mutembei akizungumza katika mahafali ya 20 ya shule ya sekondari ya St. Methew's iliyofanyika mwishoni mwa wiki shuleni hapo.
Wahitimu shule ya Sekondari ya St. Methew's akipokea cheti katika mahafali ya 20 shule hiyo.

Mwanafunzi wa shule shule ya Sekondari St. Methew's wakitoa burudani katika mahafali ya 20.
Walimu wa wakuu wa shule zinazoongozwa na Mutembei holding Limited (HML) wakiwa katika Mahafali ya 20 ya shule ya Sekondari ya St. Methew's mahafali yaliyofanyika Oktoba 3, 2020.

Wahitimu wakiwa katika mahafali ya 20 ya shule ya Sekondari St. Methew's.



Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2