IKIWA ni takribani mwezi moja tangu achaguliwa kuwa mbunge wa jimbo la Vunjo Dkt Charles Kimei, ameanza utekelezaji wa ahadi zake kwa kukabidhi sh. Milioni nne za ujenzi wa Mabweni ya wasichana ya shule ya Sekondari Ghona kata ya Kahe Mashariki.
Fedha hizo alizokabidhi ambazo ni kiasi cha shilingi milioni nne ambayo ni ahadi aliyoitoa wakati wa kampeni kuunga mkono ujenzi wa mabweni ya wasichana kwa shule ya sekondari Ghona kata ya Kahe Mashariki
Akikabidhi fedha hizo, Dkt, Kimei amesema, hiyo ni moja ya ahadi zake alizotoa wakati wa kampeni za ubunge na kuwahakikishia wananchi kuwa kwa kushirikiana na serikali, wadau wa Maendeleo na wananchi wenyewe watahakikisha wanatekeleza ahadi walizozitoa wakati wa kampeni pamoja na zilizopo kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025.
"Katika kuwathibitishia hilo leo Novemba 23,2020 nimefika kukabidhi shilingi milioni nne ambazo niliahidi wakati wa kampeni kuunga mkono ujenzi wa mabweni ya wasichana katika shule hii..., Nitaendelea kushirikiana nanyi kwa kuendelea kuchangia na kutafuta wadau wengine pia watuunge mkono ili tufanikishe ujenzi huu kwa haraka na kuwapa mabinti zetu mazingira mazuri ya kusoma. Nawaomba ushirikiano ili tuijenge Vunjo yetu kwa kasi." Amesema Dkt Kimei.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na Diwani wa kata hiyo Kulwa Kamili Mmbando, wajumbe wa bodi ya shule, walimu, wenyeviti wa vijiji kata ya Kahe Mashariki na wajumbe wa kamati ya siasa CCM kata ya Kahe Mashariki.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment