Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii
WIZARA ya mambo ya ndani ya nchi imewataka watu wote wanaotoa huduma za kidini kwa kutumia usajili wa taasisi nyingine au kigezo kuwa wanamakubaliano ya ushirika na taasisi nyingine zisizosajiliwa kuwasilisha taarifa kuhusu makubaliano ya taasisi hizo ikiwa ni pamoja na kuwasilisha nakala halisi iliyothibitishwa ya makubaliano halisi ya uendeshaji wa taasisi hapa nchini kabla ya Desemba 20,2020.
Katika taarifa ya Msajili wa Jumiaya za kijamii, wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi, Emmanuel Kihampa iliyotolewa Novemba 20,2020, imesema kuwa imebaini ongezeko la taasisi na watu binafsi ambao hawajasajiliwa na wanatoa huduma za kidini au kuendesha shughuli zinazopaswa kufanywa na tasisi zilizosajiliwa.
"Taasisi hizo zinakisingizio kuwa wanamakubaliano ya ushirika (Affilliation Agreements) na taasisi zisizosajiliwa au taasisis hizo ni matawi ya taasisi zilizosajiliwa chini ya sheria ya Jumuiya ya sura 337 kama ilifanywa marekebisho na sheria namba 2/2019."
Taarifa hiyo imesema kuwa ni kosa kitendo cha kutoa huduma za kidini bila ya kuwa na taasisi isiyosajiliwa au watu binafsi kuto huduma kwa kutumia usajili wa taasisi nyingine.
Hata hivyo taarifa hiyo imefafanua kuwa taasisi hizo ziwasilishe orodha ya matawi kwa taasisi zote zinazoendesha shughuli zake kwa kutumia utaratibu wa taasisi nyingine.
Ikumbukwe kuwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za jumuiya zikisomwa pamoja na kifungu 3.8 cha waraka wa waziri wa mambo ya ndani ya nchi wa Aprili 16, 2020 kuhusu uendeshaji wa taasisi za kidini nchini. Kuwa ninkosa kufanya shughuli za kidini bila ya kusajiliwa.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa taarifa hizo ziwasilishwe ofisi ya msajili wa jumuiya za kijamii, wizara ya mambo ya ndani ya nchi kabla ya Desemba 20, 2020.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment