Mkurugenzi Mtendaji waMamlaka ya Mbolea Tanzania (TFRA) Dkt Stephan Ngailo akipewa maelezo kutoka kwa Afisa wa Kampuni la Eka Moja Ltd linalotoa mikopo ya mbolea kwa wakulima katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi.
Wafanyakazi wa moja ya maghala ya mbolea mkoani Songwe wakishusha mbolea kwenye gari na kuhifadhi katika ghala hilo tayari kwa kuwauzua wakulima wakati huu wa msimu wa kilimo.
Pichani ni sehemu ya shehena ya Mbolea iliyohifadhiwa kwenye moja ya maghala Mkoani Mbeya
Na Mwandishi wetu
Wakulima Mkoani Mbeya watakiwa kuondoa wasiwasi kuhusu upatikanaji wa Mbolea Mkoani humo na kuwa waendele na maandalizi ya mashamba yao ili kwendana na msimu huu wa kilimo nchini.
Hayo yamesemwa na Mtendaji wa Mamlaka ya Mbolea Tanzania Dkt. Stephan Ngailo katika ziara yake kwa lengo lakujionea hali ya upatikanaji na usambaziji wa Mbolea nchini ili kuhakikisha inakidhi mahitaji ya wakulima kwenye Mikoa yote inayo jishughulisha na kilomo cha mazao mbali mbali ya chakula na biasha.
Dkt Ngailo amesema kuwa ameridhishwa na uwepo wa mbolea ya kutosha kwenye Maghala mbali mbali yaliyopo Mkoani Mbeya, huku akiwapongeza wafanyabiashara ya bidhaa hiyo kwa kufuata sherili na taratibu zote zilizowekwa na Serikali pamoja na kutoa mikopo ya mbolea kwa zaidi ya wakulima 25000 pia amekerwa na wafanya biashara wachache wanaokiuka taratibu zilizopo.
“Nimefika Mbalizi, Chunya na hapa Mbeya, nimerithishwa sana na uwepo wa mbolea ya kutosha, pia nimeridhishwa sana na uwadilifu wa wawanyabiashara ya Mbolea hapa Mbeya wanafanya kazi nzuri sana, ila nimekerwa sana na wafanya biashara wachahe, wanao kiuka utaratibu kwa kufungua mifuko ya mbolea na kuuza kwa kupima, hawa tutawashughulikia” Alisema Dkt Ngailo
Ili kuongeza tija kwenye kilimo, Dkt Ngailo amewashauri wakulima kuzingatia kanuni za kilimo bora ambacho ni pamoja na kuchagua eneo sahihi, kupanda kwa wakati, kupanda mbegu kwa usahihi pamoja na kuweka mbolea kwa husahihi na wakati sahihi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea nchini (TFRA) Dkt.Stephan Ngailo anaendelea na ziara yake ya kukagua na kujionea hali ya upatikanaji na usambaziji wa Mbolea nchini kwenye Mikoa ya Songwe, Katavi, Rukwa, Kigoma na Tabora.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment