Na Mwandishi wetu, Simanjiro
UCHAGUZI wa mgombea nafasi ya Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, kupitia CCM unatarajiwa kufanyika leo Novemba 24.
Katibu wa CCM Wilaya ya Simanjiro, Ally Kidunda amesema mchakato wa uchaguzi huo umeshakamilika hivyo wanatarajia kupata mgombea wa CCM leo Jumanne.
Kidunda amewataja watakaogombea kupitishwa nafasi ya Mwenyekiti ni madiwani wateule watatu Taiko Laizer, Albert Msole na Baraka Kanunga.
Amewataja watakaogombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti ni Diwani wa kata ya Terrat, Jackson Ole Materi na kata ya Orkesumet, Sendeu Laizer.
Diwani mteule wa kata ya Naisinyai, Taiko Laizer ameishukuru CCM kwa kumpa heshima kubwa na kurudisha jina lake kwani yeyote atakayechaguliwa ataongoza vyema Halmashauri hiyo.
Diwani mteule wa kata ya Ngorika, Albert Msole amesema yupo tayari kuingia kwenye kinyanganyiro hicho na anaishukuru CCM kwa kupitisha jina lake.
Diwani mteule wa kata ya Komolo, Baraka Kanunga amesema hana chochote cha kuzungumza zaidi ya kusubiri mchakato wa uchaguzi huo.
Wilaya ya Simanjiro ina kata 18 ambazo zote zimechukuliwa na madiwani kupitia CCM na mbunge Christopher Ole Sendeka wa CCM.
Hata hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Yefred Myenzi amewataja madiwani sita wa vitimaalum walioteuliwa na Tume ya Taifa ya uchaguzi.
Myenzi amewataja madiwani hao wateule wa tarafa sita za Wilaya hiyo kupitia CCM ni Paulina Makeseni na Bahati Patson.
"Wengine nini Mwanjaa Shirima, Rehema Zanaki, Neema Alayuni na Namnyaki Mbarnot," amesema Myenzi.
Katibu wa CCM Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Ally Kidunda.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment