Na Said Mwishehe, Michuzi TV
KATIKA kuhakikisha malengo na mikakati ya kupunguza vifo vya watoto njiti nchini, Kampuni ya simu ya Mkononi ya Vodacom kupitia kitengo chake cha kujitolea kwa Jamii ,imeamua kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Taasisi ya Doris Mollel Foundation katika kuadhimisha siku ya kuzaliwa mtoto Njiti duniani.
Maadhimisho hayo ya siku ya mtoto njiti duniani hufanyika Novemba 17 ya kila mwaka ambapo kwa mwaka huu Taasisi ya Doris Foundation imewakutanisha wadau mbalimbali kuadhimisha siku hiyo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na kuwatembelea watoto njiti waliopo Hospitali ya Taifa Muhimbili.Taasisi ya Doris Mille imejikita zaidi katika kusaidia,kufuatilia malezi ya watoto njiti kuhakikisha wanakuwa salama kama walivyo watoto wengine.
Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo ya siku ya mtoto Njiti, Meneja wa kitengo Cha kujitolea katika Kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania Sandra Oswald amesema wamekuwa wakiunga juhudi zinazofanywa na Doris Mollel Foundation wakati wote na hivyo wameamua kumuunga mkono katika harakati zinazofanywa na Doris katika kusaidia jamii na hasa ya watotp wanaozaliwa kabla ya wakati.
"Kampuni yetu yaVodacom kupitia kitengo chetu cha kujitolea kwa miaka mitano sasa tumekuwa tukishirikiana na Taasisi ya Doris Foundation katika kuwafikia wazazi ambao wanapata watoto njiti, tumekuwa tukisaidia vifaa tiba katika hospitali mbalimbali, tutaendelea na jukumu la kuendelea kusaidia jamii, " amesema.
Ameongeza kwamba Vodacom siku zote imekiwa ikitambua umuhimu wa kusaidia jamii yenye uhitaji na imeamua kushirikiana na taasisi hiyo katika kuhakikisha watoto njiti wanakuwa salama kama watoto wengine." Vodacom tumeshirikiana na jamii ya Watanzania kwa nyakati tofauti na katika eneo hili la uzazi salama na watoto njiti tumekuwa tukichangia na kiasi cha zaidi ya milioni 100 zimetumika tangu tumeanza.
"Tutaendelea kushirikiana katika kusaidia jamii kwa miaka mingine mingi ijayo.Tumeshawafikia wanawake wengi nchi kwenye mikoa mbalimbali,"amesema.
Ametaja baadhi ya mikoa ambayo wameifikia jamii ni Tabora, Katavi, Dar es Salaam, Mara, Dodoma,.Pwani Lindi,Zanzibar na Kigoma ." Tumekuwa tukishirikiana na Hospitali ya CCBRT.
"Leo hii tuko hapa kwa ajili ya kuadhimisha siku ya mtoto njiti duniani, ukweli Vodacom tunampongeza Doris Mollel kwa kazi kubwa anayofanya ikiwemo ya kuwa na taasisi hii ambayo imekita kusaidia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati. Na sisi tutaendelea kushirikiana naye na kama ilivyo kawaida ya Vodacom, tumekuwa mstari wa mbele katika kushiriki shughuli za kijamii nchini."amesema Sandra Oswald.
Kwa upande wao benki ya NCBA kupitia Meneja Msaidizi wa Benki hiyo Nasikiwa Berya amesema kwamba wamekuwa wakishirikiana na Doris Mollel katika kusaidia watoto njiti." NCBA tunasaidia jamii katika maeneo mengi kama vile eneo hilo la afya,elimu na zaidi tunashughuliza zaidi na mambo yanayohusu jamii.
"Tunampongeza Doris kupitia Taasisi yake ya Doris Foundation kwa kazi anayoifanya na wataendelea kushirikiana naye,"amesema na kusisitiza kuwa wataendelea kusaidia jamii yenye uhitaji katika maeneo yote ambayo wameyapa kipaumbele.
Amesisitiza mbali ya kusaidia jamii kwa kushirikiana na masharika na taasisi binafsi, wamekuwa wakishirikiana na Serikali katika kusaidia masuala mbalimbali na wao ni wajibu wao kuona jamii wanayoitumikia inanufaika na uwepo wapo.
Wakati huo huo Mwalinzi na Mkurugenzi wa Taasisi Doris Mollel Foundation , Doris Mollel amesema anawashukuru wadau wote ambao wamekuwa wakimshika mkono na kumtia moyo katika kuwatumikia watoto waliozaliwa kabla ya wakati huku akitumia nafasi hiyo kuwapongeza madaktari wote na wauguzi ambao wamekuwa wakiwahudumia watoto njiti.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment