Na Said Mwishehe,Michuzi TV- Dodoma
KuMEKUCHA Dodoma! Hivyo ndivyo unavyoweza kuelezea kuelekea kesho Novemba 5,2020 ambapo Watanzania na dunia itashuhudia tukio la kihistoria la kuapishwa kwa Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Magufuli.
Katika tukio hilo la uapisho , viongozi wakuu kutoka nchi 20 wakiwemo marais,viongozi wakuu wa Serikali watahudhuria.Pia kutakuwa na viongozi wastaafu pamoja na viongozi wa dini watashiriki tukio hilo ambapo mageti ya Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma yatafunguliwa kuanzia saa 12 asubuhi.
Akizungumza leo Novemba 4,2020 Mjini Dodoma , Msemaji Mkuu wa Serikali ambaye pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk.Hassan Abbas amesema maandalizi yote kuhusu sherehe za uapisho wa Rais Mteule katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma yamekamilika.
"Kwa mara ya kwanza kiapo cha Rais Mteule kitafanyika Dodoma , maandalizi yote yamekamilika na uwanja wa Jamhuri uko tayari kwa ajili ya kesho. Nchi yetu itakapokea ugeni mkubwa ssna, mpaka sasa viongozi wa wakuu wa nchi 20 wamethibitisha kuwepo.
Kwa mujibu wa Dk.Abbas miongoni mwa marais ambao wamethibitisha watahudhuria tukio hilo ni Rais wa Uganda Yower Museven, Rais wa Zimbabwe Emmason Mnangagwa pamoja na Rais wa Comoro.Pia kutakuwa na makamu wa Rais na Mawaziri Wakuu na mawaziri mbalimbali.
Pia kutakuwa na watu mashuhuri akiwemo Rais Mstaafu wa Nigeria Olesegune Obasanjo pamoja na kiongozi wa dini maarufu TB Joshua.
"Nchi mbalimbali duniani zitawakilishwa na mabalozi wao walioko hapa nchini.Mabalozi 83 wamethibitisha kushiriki,"amesema Dk.Abbas na kuongeza pia kutakuwa na wageni wa ndani.
Amefafanua wageni hao wa ndani ni pamoja na Mawaziri ambao kimsingi kwa mujibu wa Katiba baada ya Rais Mteule kuapishwa ndio watakuwa wamefika mwisho.
Hata hivyo amesema viongozi wote waliopewa kadi ya mualiko wakiwemo viongozi wote,watendaji wa mashirika ya umma na binafsi, wakuu wa idara, wakurugenzi,makatibu wakuu,majaji, na viongozi wa vyama vya siasa watapelekwa uwanja wa Jamhuri kwa mabasi maalumu.
" Wageni wote ambao wanazo kadi za mualiko , watatakiwa kuweka magari yao eneo la bustani mpya ya Chinangali kama unatokea Uwanja wa Ndege, mtu asije na gari uwanjani maana atazuiliwa , wageni ambao wataruhusiwa kufika na magari wanafahamika kwa kuanza na Rais Mteule mwenyewe."
Ameongeza mageti yatakuwa wazi kuanzia saa 12 asubuhi na kwamba tukio hilo la uapisho litakuwa na matukio makubwa mawil ambapo tukio la kwanza ni gwaride la kiapo litakaloongozwa na Majeshi ya Ulinzi na Usalama na pili kutapambwa na burudani, wasanii wote maarufu watakuwepo.
Kuhusu wananchi, Dk.Abbas amesema wanaombwa kuwahi saa 12 asubuhi ili kupata nafasi na wale ambao watakosa nafasi watakaa katika maeneo maalum yaliyoandaliwa nje ya uwanja huo.
"Hili ndio tukio la kwanza la kiserikali kikatiba na baada ya hapo yataendelea matukio mengine likiwemo la kufungua Bunge.Ratiba ya kesho inaonesha viongozi wataanza kuwasili saa mbili asubuhi,"amesema.Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa leo Novemba 4, 2020 ametembelea na kukagua maandalizi ya Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma utakaotumika kwa ajili ya uapisho wa Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli utakaofanyika tarehe 5 Novemba, 2020.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment