MAFANIKIO YALIYOPATIKANA MIRADI YA USIMAMIZI SHIRIKISHI WA MISITU YA JAMII YAWAKOSHA USWISI | Tarimo Blog

Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Iringa

MAFANIKIO ambayo yamepatikana kupitia miradi ya Usimamizi wa Shirikishi wa Misitu ya Jamii Tanzania(USMJ) inayotekelezwa na Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania(TFCG) pamoja na Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania(MJUMITA) umewaridhisha wafadhili wa mradi huo ambao ni nchi ya Uswisi.

Miradi hiyo inafadhiliwa na  Shirika la Maendeleo la Uswisi (SDC) na kuratibiwa na Shirika la Kuhifadhi Misitu Asili Tanzania (TFCG), Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA) na Shirika la Kuendeleza Nishati Tanzania (TaTEDO).

Mkuu wa Idara ya Ajira na Kipato kutoka Ubalozi wa Uswisi, Peter Sidler amesema wao kama wafadhili wa miradi hiyo wameridhishwa na wanafurahishwa na namna ambavyo imekuwa na mafanikio makubwa katika maeneo yote ambayo miradi inatekelezwa

"Ushirikiano wa Tanzania na Uswisi una zaidi ya miaka 30 , matarajio yetu ni kuendeleza hasa kwa kugusa kundi kubwa la jamii vijijini.Takwimu zinaonesha Tanzania ni moja ya nchi zinazoongoza kwa uharibifu wa misitu.Hivyo miradi ya USMJ inayotekelezwa inapaswa kuungwa mkono ili kukabiliana na madhara ya mabadiliko ya tabia nchi.

"Shughuli  za uhifadhi zinazofanyika Kijiji cha Mahenge zimeonesha picha nzuri kuwa jamii ipo tayari kutunza na kuhufadhi misitu yao na kunufaika hivyo wataendelea kuwezesha taasisi kama TFCG na MJUMITA ili kuendeleza malengo ya wanavijiji,"amesema na kushauri ni vema katika kuhakikisha miradi hiyo inafanikiwa jamii nayo iatakiwa kushiriki kikamili.

Aidha amesema wao Serikali ya Uswisi wanasaidia sehemu kidogo ya ufadhili wa uhifadhi na kuboresha maisha ya wananchi lakini jukumu kubwa lipo chini ya Serikali na wananchi wenyewe.Hivyo amesisitiza umuhimu wa wadau wote wakashirikiana ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi. 

Amesisitiza wataendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania kuhakikisha sekta zote zinahusika katika kuondoa umaskini huku akieleza Tanzania imejaliwa misitu mingi ambayo ikitunzwa vizuri itaweza kuchochea uwepo wa hali ya hewa nzuri.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania(MJUMITA) Rahima Njaidi amesisitiza kuwa wao na TFCG wameweka mikakati ya dhati katika kuhakikisha malengo ya uhifadhi wa misitu na utunzani mazingira yanafanikiwa.

Wakati huo huo Mkurugenzi wa TFCG Charles Meshack ameeleza kwa sasa nchini Tanzania kuna hekta milioni 48.8 za misitu ambapo hekta milioni 22 ipo katika ardhi za vijiji na hekta milioni 5 ndio ipo kwenye USMJ huku hekta milioni 17 hazipo katika usimamizi.

"TFCG na MJUMITA tumeamua kuja na mradi wa TTCS NA CoFoREST kwa ajili kuwezesha wananchi kutambua umuhimu wa utunzaji wa misitu.Iwapo hakutakuwa na jitihada za kuhifadhi misitu ni wazi katika kipindi cha miaka 40 ijayo misitu itatoweka,  takwimu zinaonesha hekta 469,000 kila mwaka  zinapotea." Amesema.

Ameongeza miradi hiyo ambayo tunawapelekea wananchi ina malengo makuu matatu ambayo ni kuhamasisha wananchi kuhifadhi misitu ya asili na kuvuna kwa uendelevu na wanapovuna kwa undelevu kipato wawekeze kwa shughuli za wananchi na uhifadhi.Kusaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ili nchi isiwe jangwa. 

"Lengo kubwa ni kuwapa wanavijiji motisha wananchi wasigeuze misitu mashamba badala yake waweze kuvuna kwa uendelevu mkaa na mbao." Amesema.

Amesisitiza miradi ya USMJ ambayo wameibua kwa takribani miaka saba sasa imechochea maendeleo, kuchochea uhifadhi na kukuza uchumi huku akifafanua katika vijiji zaidi ya 30 ambavyo vinatekeleza mradi vimeweza kuboresha sekta ya elimu, afya, maji, kilimo na mikopo."Ambapo wanavijiji wamekusanya zaidi shilingi bilioni 3.

Meshack amesema kwamba wamewekeza Sh. bilioni 12 katika awamu ya kwanza na pili lakini.Pia zaidi ya Sh.bilioni 3 zimepatikana."Awamu hii ya tatu tunatarajia kuwekeza Sh.bilioni 7 katika kipindi cha miaka mitatu na kwamba wamejikita kuwajengea uwezo wataalam ili waweze kutekeleza zenyewe.

Aidha amesema kupitia miradi hiyo wamefanikiwa kurasimisha ardhi za vijiji kuwa za kisheria jambo ambalo linatoa uhakika wa kupangia kazi kisheria na kwamba Serikali inapaswa kutoa kipambele katika sekta ya mazingira na misitu ili iweze kuwa endelevu na kuondoa sheria vikwazo katika kusimamia misitu akitolea mfano GN417.

Wakati huo huo Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, Elia Luvanda ametoa shukrani kwa nchi ya Uswisi, TFCG, MJUMITA na wadau wengine ambao wamekuwa mstari wa mbele na kutambua umuhimu wa kuhifadhi na kutunza mazingira.

Kwa upande wa Mtafiti Mwandamizi wa Taasisi ya Utafiti Tanzania (TAFORI), Dk.Charlestino Balama ametumia nafasi hiyo kuwashauri wataalam na wananchi kutafuta watafiti ili kubaini fursa zote zilizopo katika misitu wa Kijiji cha Mahenge.

Mkurugenzi Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania(MJUMITA) Rahima Njaidi akizungumza jambo wakati wa kikao hicho.

Kuanzia kushoto ni Mkurugenzi wa Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania(TFCG)Charles Meshack, Mkurugenzi Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania(MJUMITA) Rahima Njaidi na Meneja wa Mradi wa CoForEST) Charles Leonard wakiwa makini kufuatilia maelezo yaliyokuwa yakitolewa na wadau wakati wa kikao kilichofanyika Kijiji cha Mahenge.

Kulia ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Elia Luvanda akizungumza mbele ya wadau wa uhifadhi wa misitu na mazingira.Aliyekaa ni Mkurugenzi wa Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania(TFCG)Charles Meshack.

Mkuu wa Idara ya Ajira na Kipato kutoka Ubalozi wa Uswisi nchini Tanzania Peter Sidler(kulia)akiwa na maofisa wengine wakijadiliana jambo kabla ya kuingia katika Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Iringa.

Maofisa kutoka idara mbalimbali za Serikali zinazohusika na masuala ya misitu na uhifadhi wa mazingira wakijadiliana jambo kabla ya kuanza safari ya kwenda kijiji cha Mahenge wilayani Kilolo mkoani Iringa ambako mradi wa kuhifadhi misitu kwa kuwezesha biashara endelevu ya mazao ya misitu tanzania unatekelezwa.

Mkuu wa Idara ya Ajira na Kipato kutoka Ubalozi wa Uswisi nchini Tanzania Peter Sidler(kulia) akifutia kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Iringa Elia Luvanda(hayupo pichani).Joan Kushoto ni Mshauri Mkuu wa Mradi wa FORVAC Juhani Harkonen, Ofisa Miradi wa ubalozi wa Uswisi Clara Melchior na kulia ni Ofisa Maliasili Mkoa wa Morogoro Jeseph Chuwa. 
Mkurugenzi Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania(MJUMITA), Rahima Njaidi akifafanua jambo mbele ya Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Iringa Elia Luvanda(hayupo pichani) wakati wa kikao cha utambulisho.
Mkurugenzi wa Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania(TFCG)Charles Meshack (aliyesimama) akizungumza kuhusu umuhimu wa uhifadhi wa misitu ya asili kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kupitia miradi wanayoifadhili katika Kijiji cha Mahenge wilayani Kilolo mkoani Iringa.Kulia ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Iringa Elia Luvanda na kulia ni Ofisa Maliasili Mkoa wa Morogoro Joseph Chuwa.
Wadau wa uhifadhi wa misitu na mazingita wakiwemo Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania(TFCG) Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania(MJUMITA), maofisa wa idara mbalimbali za mazingira kutoka serikalini pamoja na maofisa wa ubalozi wa Uswisi wakiwa katika picha ya pamoja na wananchi wa Kijiji cha Mahenge ambako mradi wa kuhifadhi misitu kwa kuwezesha biashara endelevu ya mazao ya misitu Tanzania(CoForEST).
Wadau wa uhifadhi wa misitu na mazingita wakiwemo Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania(TFCG) Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania(MJUMITA), maofisa wa idara mbalimbali za mazingira kutoka serikalini pamoja na maofisa wa ubalozi wa Uswisi wakiwa katika kikao cha utambulisho baada ya kufika ofisini kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2