MAFUNDI manispaa ya Songea wasikitishwa na kitendo cha mtoto Hamisi Rashidi (9) kuuza matembele asubuhi namapema huku akionekana amechoka hajala na akipepesuka na kuendelea na safari ya kuuza mboga,
Wakimhoji mtoto Rashidi akiwa na mboga yake mafundi wanaofanyia kazi zao eneo la kauru Fundi peter na fundi Rolandi walidai walilazimika kumsimamisha mtoto huyo na kisha kumpatia hela ya kumnunulia uji ilia pate nguvu ya kuuza mboga hiyo ya Matembele
Kwa mujibu wa maelezo ya mtoto mwenyewe Hamisi alidai mama yake na baba walitengana akiwa mtoto mdogo na wakamwacha yeye kwa bibi yske anayeishi Bombambili manispaa ya Songea na toka wazazi wake wamemwacha hajawahi kuwaona.
Mtoto Hamisi alisema mama yake anaambiwa na bibi yake kuwa anaishi mbinga na baba yake anaishi kijiji cha mchomoro katika Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo aliyemtaja kwa jina la Rashidi Ramadhani.
Hamisi alipoulizwa juu ya kumfuata baba yake aliko alisema hajawahi kumwona zaidi ya kuambiwa na bibi yake aliyemtambulisha kwa jina la binti Hasani kuwa baba yake alikuwa anaishi na mama yake akitokea kijiji cha mchomoro lakini hajawahi kumwona baba yake huyo zaidi ya kusimuliwa na bibi yake huyo
Mafundi manispaa ya songea licha ya kumwonea huruma mtoto huyo ambaye kwa umri wake alitakiwa kuwa anaendelea na masomo lakini kutokana na mazin gira anayoishi bibi yake huyo hana uwezo wa kumnunulia mahitaji yakumfanyia asome shule na badala yake anahangaikia kuuza mboga ili waweze kupata chakula na na bibi yake ambaye naye ni mzee hawezi kufanya biashara .
Wazazi wa hamisi walitengana katika maisha yao na kwa kipindi hicho mtoto huyo alikuwa mdogo kiasi ambacho hakuwatambua na walimwacha kwa bibi yake na kulelewa na bibi yake huyo kwa njia ya kuuza mboga na sasa kazi hiyo ya kuuza mboga bibi yake amemhamishia mtoto huyo kutokana nay eye kukosa uwezo wa kutembea alisimulia mtoto huyo.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment