MAMLAKA ya Hali ya Hewa nchini (TMA), imetoa tahadhari ya kuwepo kwa mvua kubwa kesho Novemba 24,2020 kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Dar es Salaam, Pwani(Ikijumlisha visiwa vya Mafia) na Lindi.
Taarifa ya TMA iliyotolewa leo Novemba 23, 2020 ya Utabiri wa siku tano imesema mvua hiyo ya kesho inaweza kusababisha athari mbali mbali ikiwa ni pamoja na baadhi ya makazi kuzungukwa na maji pamoja na kuathirika kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi huku ikisisitiza wananchi kuzingatia agizo hilo pamoja na kujiandaa.
Hata hivyo, TMA katika taarifa yake hiyo umesema, hali ya hewa kwa siku tano kuanzia Novemba 23 imeonesha kuwepo kwa hali ya kawaida ya hewa kwa siku nyingine isipokuwa kesho.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment