Mkurugenzi wa Msafiri Travel na Mjasiliamali, Leina Lemomo akizungumza kwenye 'Kongamano la Woman of Influence, I'm Possible' kwenye Hotel ya Serena Dar es Salaam. Kongamano hilo pamoja na mambo mengine lilijadili namna wajasiriamali wanawake walivyo kabiliana na changa moto za janga la corona kwenye biashara zao.
Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii
ILI kuhakikisha soko la Utalii kwa nchi za Afrika liwezekukua latakiwa kuwa na kiwango cha fedha za utalii kwa Afrika nzima (African Rates) ambazo zitasaidia waafrika kutembelea vivutio vilivyopo barani.
Hayo aliyasema Mkurugenzi wa Msafiri Travel, Leina lemomo wakati akizunngumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. Alisema kuwa bara la Afrika nalo linawatalii wengi lakini tatizo ni kuwa na viwango tofauti kwa vya kuingilia katika sehemu za vivutio vilivyomo barani.
“Afrika kama bara na Tanzania kama Nchi hatujawahi kuangalia utalii wa ndani lakini kwa miaka mingi ambapo utalii unaendelea hatujawahi kuwa na kiwango cha Fedha (African Rates)au gharama ambazo zinavutia waafrika kutoka bara nzima la Afrika."
Ukiangalia kwenye soko la Utalii unaona kuna viwango tofauti tofauti ambavyo ni (Italian Rates, English Rates, American Rates, Russia rates na Polish rates), kwa Afrika nzima ukiangalia hatujawahi kuwa na viwango vya Utalii.
Ingawa kunaviwango mbalimbali vya kanda lakini kwa sasa ni zamu ya Bara laAfrika Kupanfa viwango hivyo ili vimwezeshe kila Mwafrika Kutembelea Vivutio vya Afrika Nzima." Alisema Leina.
Kuna kanda mbalimbali ambazo zinaambazo zimeweka viwango vyao vya utalii mfano Afrika Mashariki ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda na Sudani kusini wazawa wa Afrika Mashariki wananufaika na viwango hivyo, ukienda nchi za Afrika Magharibi ambazo ni
Benin, Burkina Faso, Cape Verde, Ivory Cost, Gambia, Ghana, Guinea, Guinea-Bissau, Liberia, Mali, Niger, Nigeria, Senegal, Sierra Lieoni na Togo (ECOWAS), Unapata viwango vya utalii vya (ECOWAS Rates) na Ukienda nchi za Kusini mwa Afrika unakuta (SADC Rates) Viwango hivyo vyote ni kwa nchi za kanda.
Na mtu kutoka nchi nyingine ambaye hajui viwango vya bei za utalii akienda kutalii vivutuo vilivyopo nchi nyingine analipishwa kama mzungu ambaye anakiwango chake cha utalii.
“Sasa hii Taasisi yetu ya Intra Africa Traveller Vature fare Initiative lengo letu ni kuhakikishatunahamasisha watoa huduma za utalii ambao ni ‘Camps’, mashirika ya Ndege na hoteli ziweze kutoa viwango ambavyo tutaita na sisi ‘African Rates’(Viwango vya fedha za Utalii kwa Afrika).” Alisema Leina.
Licha ya hayo watoa huduma za utalii wakishatoa viwango hivyo vya Utalii kwa kwa nchi za bara la Afrika ambapo zitaunganishwa na Viwango vingine vya mabara mengine katika utalii wa wazawa wa Afrika.
Leina Amesema kuwa ili kuhakikisha utalii wa wazawa wa Bara la Afrika linakuwa zaidi kama nchi za mabara mengine.
“Soko la Utalii liweze kugundua kuwa waafrika naowanaweza kusafiri kwenda kwenye vivutuo vilivyopo barana. Kama nasisi tutakuwa na gharama nafuu kwaajili ya kutalii katika vivutio vilivyopo barani mwetu.” Amesema Leina.
Leina amesema kuwa nchi zaidi ya 12 za bara la Afrika walishiriki katika Mkutano wa Mtandaoni (Video Conference) na watu zaidi ya 125 walishiriki kikamilifu kutoa maoni yao juu ya kushirikiana pamoja kupanga Viwango vya fedha za Utalii za Bara la Afrika.
Alisema kuwa kila nchi ilionesha kuwa inakivutio gani cha utalii ambacho kitamwezesha mzawa wa Bara la Afrika kutembelea nchi za Bara hili.
“Waliohudhulia mkutano huo wengi walisema hawakujua kama Bara la Afrika linavivutio vizuri kama tulivyoongea leo sasa inatakiwa tuvitembelee.” Alisema Leina.
Hata hivyo Leina alisema kuwa waliendelea kuongea na watoa huduma mbalimbali za utalii katika bara nzima la Afrika kwaajili ya kuangalia ni namna gani watashirikiana katika kupanga viwango vya mzawa wa bara la Afrika.
Alisema kuwa kila aliyeshiriki mkutano wa mtandaoni alikubali kuanzisha Viwango vya Fedha za utalii kwa wazawa wa Bara la Afrika (Afrikani Rates).
Mafanikio
Kwa hapa nchini kampuni ya kwanza kuanzisha Viwango vya Utalii kwa wazawa wa Bara la Afrika ni Coastal Aviation na ukiangalia kwenye tovuti vya Coastal Aviation wao wanaviwango vya fedha za Utalii kwa wazawa wa Bara la Afrika, hii inamanisha kuwa kwa mwafrika yeyote anayekuja Tanzania akitaka kutembelea Vivutio vya Tanzania anakutana na Viwango vya utalii vya Afrika (African Rates).
Ukitembelea Vivutio vya Afrika ya Kusini wao wanaviwango vya Utalii kwa mzawa wa Bara la Afrika (African Rates), Kwa Tanzania kunabaadhi ya kampuni kama Msafiri Travel na baadhi ya hoteli kama Ramada nao wanaviwango vya Utalii va Kiafrika.
Changamoto
Changamoto kubwa iliyopo Leina alisema kuwa Waafrika tunashindwa kusafiri katika Bara la Afrika kutokana na gharama kubwa za huduma za utalii.
Hata hivyo Leina amewahamasisha wazawa wa Bara la Afrika wote wanaposafiri kutembelea vivutio vya barani Afrika, kuulizia viwango vya fedha za utalii(Africa Rates) na wasiogope kuuliza gharama za utalii za Kiafrika.
0659481912
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment