NAWASHUKURU MASHABIKI KWA KUNISAPOTI NDANI YA MIAKA 10- BEN POL | Tarimo Blog


Msanii wa Muziki wa R &B Behman Paul ' Ben Pol'

Na Mwandishi Wetu. Dar 

MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Flava Benham Paul 'Ben Pol' amewashukuru mashabiki wake kwa Kumpa ushirikiano kila anapotoa nyimbo yake mpya.

Ben Pol ameachia wimbo wake mpya ujulikanao kama Hiyo ndio Mbaya. 

Amesema amekuwa akipata ushirikiano kutoka kwa mashabiki wake hivyo ujio wa muziki wake huo mpya ambao ameutoa kwa staili ya Singeli.

"Nashukuru kwa sapoti ninayopata kutoka kwa mashabiki zangu na wadau , sasa nina miaka 10 kwenye muziki wamekuwa na mimi bega kwa bega, sasa nimekuja na wimbo katoka staili ya singeli unaitwa "Hiyo ndio Mbaya" 

Amesema wimbo huo amemshirikisha msanii mpya Tamimu, wa kiufanyia katika ya Pizzey Records, chini ya Mtayarishaji (Producer) Jay Stereo, 

"katika kuelekea kufunga mwaka nitatoa wimbo mpya kila wiki, mashabiki zangu wajiandae kupokea kazi zangu", amesema 

Pia amesema ameanza kuzunguka mikoani kufanya matamasha ya kuwashukuru mashabiki zake akianzia Mkoa wa Mbeya , mikoa mingine inafuata naomba wampokee.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2