Rais wa Tanga' ahukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 30 jela | Tarimo Blog

Mshtakiwa Yanga Omary Yanga, maarufu kama 'Rais wa Tanga' akiwa katika ukumbi wa wazi wa mahakama Kuu kitengo cha makosa ya rushwa na uhujumu uchumi, Kanda ya Tanga, baada ya kuhukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 30 gerezani kwa kupatikana na hatia katika kosa la kusafirisha gramu 1052.63 za dawa za kulevya huki mke wake Rahma Juma wa kati kati na mfanyakazi wao wa ndani Halima Mohamed wakiachiwa huru
Mshtakiwa Yanga Omary Yanga, maarufu kama 'Rais wa Tanga'  akitoka ukumbi wa wazi wa mahakama Kuu kitengo cha makosa ya rushwa na uhujumu uchumi, Kanda ya Tanga, baada ya kuhukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 30 gerezani kwa kupatikana na hatia katika kosa la kusafirisha gramu 1052.63 za dawa za kulevya.

MAHAKAMA Kuu, Kitengo cha Rushwa na Uhujumu Uchumi, imemhukumu mfanyabiashara maarufu jijini Tanga, Yanga Omary Yanga,(Mwenye kazu nyeupe) maarufu kama 'Rais wa Tanga' kutumikia kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia katika kosa la kusafirisha gramu 1052.63 za dawa za kulevya aina na herion.

Hukumu hiyo imesomwa leo Novemba 20, 2020  na Jaji Imakulata Banzi aliyekuwa anasikiliza shauri hilo katika Mahakama Kuu, Kanda ya Tanga,  baada ya mshtakiwa kutiwa hatiani kufuatia ya kuridhishwa ushahidi uliotolewa na mashahidi wa upande wa mashtaka.

Akisoma hukumu hiyo Jaji Banzi amesema, upande wa mashitaka ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu Faraja Nchimbi kupitia mashahidi saba na vielelezo kumi vilivyowasilishwa mahakamani hapo wameweza kuthibitisha bila kuacha shaka yoyote kuwa mshtakiwa Yanga alikuwa akijihusisha na biashara hiyo haramu ya madawa ya kulevya.

“Kwa kuzingatia ushahidi huo, mahakamahii inamtia hatiani mshitakiwa kwa kosa la kusafirisha dawa za kulevya kama alivyoshitakiwa.” Amesema Jaji Banzi.

Kabla ya mahakama kutoa adhabu, upande wa mashitaka uliiomba mahakama kuzingatia uzito wa kosa na adhari za madawa hayo katika jamii na katika kuathiri uchumi wa nchi. Hata hivyo, upande wa utetezi uliomba adhabu nafuu itolewe kwa mshtakiwa kwa vile ni mkosaji wa kwanza na anafamilia inayomtegemea.
 
Hata hivyo Mahakama imemuachia huru mke wa Yanga, Rahma Juma na mfanyakazi wao wa ndani Halima Mohamed, baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha kesi dhidi yao.

Akieleza zaidi juu ya kuachiwa kwa wawili hao, Jaji Banzi amesema kuwa upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha shtaka hidi yao kwa vile tangu mwanzo taarifa kuhusu kutendeka kwa kosa hilo zilitolewa zikimhusisha mshitakwa wa kwanza (Yanga) pekee.

Amesema kuwa mshtakiwa Rahma hakuhusishwa kwa namna yoyote tangu mwanzo na kwamba mshtakiwa Halima alikuwa mfanyakazi wa ndani na vitu vilivyokutwa kwenye chumba chake vilithibitika havikuwa  ya kulevya.

Mawakili wengine waliokuwa wanaiwakilisha jamhuri katika shauri hilo ni Wakili Mwandamizi Pius Hilla, Mawakili wa Serikali Constantine Kakula, Salimu Msemo, Donata Kazungu na Mseley Mfinanga, ambaye ni mwanasheria mwandamizi kutoka Mamlaka ya Kuzuia Dawa za Kulevya (DCEA) na washitakiwa walikuwa wanawakilishwa na Mawakili Majura Magafu, Nehemia Nkoko, Mohamed Kajembe, Kahoza Nicholaus na Denis Tumaini. 

Katika kesi ya msingi  inadaiwa Oktoba 1, 2018 huko atika eneo la Bombo Jijini Tanga washtakiwa walikamatwa wakisafirisha gramu 1052.63 za dawa za kulevya aina ya Heroin Hydrochloride.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2