Na Mwandishi Wetu
SHULE ya Msingi Hazina ya jijini Dar es Salaam imempongeza Rais Dk. John Magufuli kwa ushindi mkubwa alioupata kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa ya shule hiyo iliyotolewa na Mkuu wa shule hiyo, Juma Omari ushindi huo umedhihirisha namna watanzania wanavyomkubali kutokana na utendaji kazi wake uliotukuka.
Imesema Rais Magufuli tangu aingie madarakani Novemba 2015 ameifanyia nchi mambo makubwa hali ambayo imeongeza imani kwa wananchi kuwa ni kiongozi bora hivyo kumchagua kwa kura nyingi ili aongoze kwa muhula mwingine.
Imeongeza kuwa, Rais Magufuli ameipa kipaumbele sekta ya elimu kwa kutoa elimu bure kwa watoto wa watanzania na kuhakikisha sekta hiyo inazidi kukua siku hadi siku kwa kushirikiana na sekta binafsi.
“Sisi wadau wa elimu wa sekta binafsi tumefurahishwa sana na ushindi wa kishindo wa Rais Dk. Magufuli kwasababu serikali ya awamu ya tano imetufanyia mengi mazuri na imekuwa ikitoa ushirikiano sana kwa sekta binafsi upande wa elimu,” ilisema
Taarifa hiyo imeendelea kusema kuwa, shule hiyo inaimani kubwa na Rais Magufuli kwamba licha ya kuiendeleza nchi kimiundombinu itaendelea kushirikiana na sekta binafsi upande wa elimu ili kuikuza sekta hiyo kwa manufaa ya watanzania wote.
Imesema wadau wa elimu sekta binafsi wamekuwa na mchango mkubwa kwenye sekta ya elimu hivyo wanaomba ushirikiano uliopo baina ya sekya ya umma na binafsi uendelezwa kwa manufaa ya watanzania wote.
Mdau mwingine wa elimu kutoka shule ya msingi Precious ya Mbagala, John Mapunda amesema sekta binafsi upande wa elimu wanamengi ya kujivunia kutokana na uongozi mahiri wa Rais John Magufuli.
“Kwa upande wa elimu amefanya mengi makubwa ambayo tunaamini kwa kupewa miaka mingine mitano ataendeleza yale mazuri tuliyoyapata awamu iliyopita,” alisema Mapunda
Rais Magufuli anaapishwa kesho mkoani Dodoma baada ya kushinda kwa kishindo kwa kupata kura milioni 12.5 kwenye ichaguzi uliopita huku anayefuata akipata kura milioni 1.9.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment