Katibu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya amesema, watanzania wategemee mageuzi makubwa katika kilimo cha umwagiliaji, kwani serikali ya awamu ya tano imejipanga kikamilifu kukabiliana na changamoto zinazoikabili sekata hiyo.
Bw. Kusaya ameyasema hayo jijini Dodoma alipokuwa na ziara ya kikazi katika ofisi za Tume ya Taifa yaUmwagiliaji, ambapo amesema Serikali ina mpango wa kuboresha mundombinu yote chakavu katika sekta ya umwagiliaji na kufufua skimu za zamani na kuongeza skimu mpya.
Alisema pia ikiwemo kuongeza vyanzo vipya vya maji katika maana ya kujenga mabwawa na kutumia vyanzo asili vilivyopo kama mito, mabwawa ya asili na maziwa hivyo mkulima atanufaika na kilimo cha umwagiliaji katika mazao ya biashara na chakula.
Sambamba na hilo, amesema Serikali pia imeona umuhimu wakuongeza wataalamu wa sekta hiyo katika ngazi za wilaya na itafikia ngaz iya kata na kijiji ili kuweza kumfikia mkulima kwani kilimo cha umwagiliaji ndicho kilimo cha uhakika na mkombozi kwa mkulima.
“wakulima watapata huduma za uhakika zaidi na kunufaika na kilimo cha umwagiliaji” Alilisita.
Awali, alipokuwa akizungumza na menejimenti yaTume ta ya Taifa ya Umwagiliaji, Bw. Kusaya amewataka watumishiwa Tumeya Taifa ya umwagiliaji kufanya kazi kwa ushirikiano,na uhakika ili kuweza kufikia malengo ya mageuzi makubwa yenye tija katika sekta ya umwagiliaji.
Na baada ya hapo katibu Kusaya alikagua mitambo iliyopo katika ofisi za Tume hiyo inayotumika kujengea na kuboresha miuondombinu ya umwagiliaji.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment