Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
KAMPUNI ya Airlink inayoshughulika na masuala ya usafiri wa anga leo Desemba 23 imejumuika na watoto yatima kutoka kituo cha Kibaha Orphanage Centre kwa kupata kupata chakula pamoja na kutoa misaada mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kusherehekea msimu wa sikukuu sambamba na kurudisha fadhila kwa jamii.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkazi wa Airlink Tanzania, Robert Othman amesema kuwa kampuni hiyo imeanza kufanya kazi rasmi Desemba Mosi mwaka huu na wateja na jamii kwa ujumla kwao ni watu muhimu sana wakati wote.
"Tumeanzaa kazi Desemba mwaka huu na katika msimu wa sikukuu tumekutana na watoto yatima kutoka Kibaha Orphanage Centre, tutakula nao pamoja na kuwapa chochote kitu, na hii ni sehemu ya majukumu yetu katika kukuza biashara bora ya anga na jamii kwa ujumla." Amesema.
Aidha amesema kuwa kampuni, taasisi na wanajamii wajitoe kuwasaidia watoto waishio kwenye mazingira ya magumu kwa kuwapa mahitaji muhimu ya kimaisha.
Vilevile mmoja wa watoto hao Imani Mussa ameishukuru Airlink kwa kuwakumbuka katika msimu huu wa sikukuu.
"Tumefurahi, tunawashukuru sana kwa kutukumbuka na kutuita hapa leo na kutupa baadhi ya matumizi, Mungu awabariki." Amesema.
Kampuni ya Airlink inayoshughulika na masuala ya usafiri wa anga kwa safari za Tanzania na Afrika Kusini ilianza rasmi safari zake Desemba Mosi mwaka huu na imedhamiria kurudisha fadhila kwa jamii kupitia mradi huo.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment