Na Eliud Rwechungura
Ikiwa ni mwaka mmoja baada ya kuondokewa na Mzee Nekemia Musa Kazimoto, Leo tarehe 23 Disemba 2020 Familia ya Mzee Kazimoto imefanya ibada ya shukrani ya kumbukumbu ya mwaka mmoja ya kumuombea mzee wao, ibada hiyo imefanyika nyumbani Omugakorongo, Karagwe, Kagera.
Nekemia Musa Kazimoto alizaliwa mwaka 1937 katika kijiji cha Nyakahanga, Wilaya ya Karagwe, Mkoa Kagera na alifariki Mwezi Disemba 2019 na kuzikwa nyumbani kwake Kayanga, Karagwe tarehe 23 Disemba 2019.
Mzee Kazimoto aliwahi kufanya kazi katika mashirika ya umma, Serikalini na vyama vya wafanyakazi hadi kuwa Rais wa Tanzania Federation of Labour (TFL), alikuwa mfanyabiashara aliyefanikiwa, mkulima na mfugaji bora. Pia, amewahi kuwa mwenyekiti wa Chama kikuu cha Ushirika cha Wilaya ya Karagwe, taasisi na asasi za dini na zisizokuwa za Serikali.
Mzee Nekemia Kazimoto aliwapa wosia wanaoukoo na wasomaji wake hasa watoto wake kumi na nne (Saba wa kike na saba wa kiume) na mke mmoja kwa kuandika kitabu cha hitoria yake kiitwacho "Maisha na Harakati za Kazimoto"
"Nawaomba sana mpokee wosia huu kwa wapenzi, kwani mimi nikiwa kama mwenzenu, mzazi, babu, rafiki, niite vyovyote upendavyo, nimebahatika kama wengine wengi, kuishi zaidi ya miaka sabini ulimwenguni hapa. Nimepata raha nyingi na shida za hapa na pale ikiwa ni sehemu ya maisha ya binadamu. Sijutii kwa lolote kwani nakubaliana na mafundisho ya dini yasemayo Mwenyezi Mungu ndiye muumba wetu, mpangaji na kiongozi wa maisha yetu, hivyo tumshukuru Kwa kila jambo" aliandika Mzee Nekemia Kazimoto katika kitabu cha Maisha na Harakati za Kazimoto.
Wakati akiongoza ibada shukrani Mchungaji wa Kanisa la KKKT wa usharika wa Kanyanga, Mch. Jovinali Karoro ameleza mambo mengi aliyoyafanya mzee Nekemia kazimoto huku akiwataka ndugu na jamaa kuyaishi mambo na matendo mema aliyoyafanya wakati wa uhai wake ambapo alikuwa mcha Mungu na Kiongozi katika Kanisa.
"Wapendwa leo tunahitimisha maombolezo na sasa tuna safari nyingine mpya kuanzia leo na safari hii ni hasa ya kuenzi mambo mazuri ya mzazi wenu aliyojishughulisha nayo mpaka maisha yake alipokoma hapa duniani na nipande kutaja machache tu, jambo la kwanza alijivunia sana ukristo wake mpaka ametwaliwa alikuwa mkristo hai mwenye msimamo na imani yake, jambo la pili alijishughulisha sana na na kutumia vizuri wakati wake katika kuzalisha bila kupoteza wakati, jambo la tatu alipenda sana kudumisha umoja ndani na nje ya familia na kanisa pia, mzee huyu hakuwa na tabia ya kutangatanga" Anesema Mchungaji Karoro.
Nae Florence Wamara, mke wa Nekemia Kazimoto amepata nafasi katika ibada ya kutoa shukrani kwa Mwenyezi Mungu kwa neema ambayo ameendelea kuijalia familia yake tangu kuondokewa na mzee wao amezidi kutoa shukrani kwa ndugu, jamaa na majirani kwa kuendelea kuwa karibu na familia yao
"wana wa Mungu mliofika leo hapa tunawashukru sana mmetuonesha upendo wenu, siku ya msindikiza baba yetu mzee Kazimoto tuliona umati mkubwa kutoka pande zote kuja kuungana na kuomboleza nasi, hatujapata nafasi ya kumshukru kila mmoja ila itoshe kusema asanteni nyote kwa kila namna mlivyojitoa na Mungu wa Majeshi hatawapungukia" amesema mama Florence.
Kwa upande wake Mzee Clement Nsherenguzi aliyekuwa rafiki wa karibu amepata nafasi ya kuyaeleza maisha halisi ya mzee Kazimoto huku akieleza namna walivyoishi wote kwa upendo
"Mimi natoa shukrani zangu kwa Mungu kwa sababu niliondokewa na pacha wangu, Kazimoto nilikuwa namzidi mwaka mmoja lakini katika maisha yangu zaidi ya 90% ameniongoza na kunilea yeye maana tumejuana kwa miaka 75 tangu mwaka 1944 tukiwa watoto wadogo" Ameshema Mzee Nsherenguzi.
Picha ya Marehemu Nekemia Musa Kazimoto katika ibada ya shukrani iliyofanyika leo tarehe 23 Disemba 2020 ikiwa ni mwama mmoja baada ya kutwaliwa kwake, alizaliwa mwaka 1937 katika kijiji cha Nyakahanga, Wilaya ya Karagwe, Mkoa Kagera na alifariki 19 Disemba 2019 na kuzikwa nyumbani kwake Kayanga, Karagwe tarehe 23 Disemba 2019. Mchungaji Jovinali Karoro wa Kanisa la kiijiri la Kirutheli Tanzania KKKT usharika wa Kayanga akiongoza ibada ya shukrani ikiwa ni mwaka mmoja baada ya kutwaliwa kwa Mzee Nekemia Musa Kazimoto, ibada hiyo imefanyika nyumbani kwake Omugakoroho, Kayanga Karagwe. Leo tarehe 23 Disemba 2020 Mama Florence Wamara, mke wa Nekemia kazimoto (katikati) akitoa shukrani kwa Mwenyezi Mungu kwa neema ambayo ameendelea kuijalia familia yake tangu kuondokewa na mzee wao, katika ibada ya shukrani ikiwa ni mwaka mmoja baada ya kutwaliwa kwa Mzee Nekemia Musa Kazimoto, ibada hiyo imefanyika nyumbani kwake Omugakoroho, Kayanga Karagwe. Leo tarehe 23 Disemba 2020. Kulia ni Florence Kazimoto, Mtoto kwa kwanza wa Mzeee Nekemia, Kushoto ni Getrode Jacob. Mzee Clement Nsherenguzi (kulia) aliyekuwa rafiki wa karibu Mzee Nekemia Kazimoto akiyaeleza maisha halisi ya mzee Kazimoto katika ibada ya shukrani ikiwa ni mwaka mmoja baada ya kutwaliwa kwa Mzee Nekemia Musa Kazimoto, ibada hiyo imefanyika nyumbani kwake Omugakoroho, Kayanga Karagwe. Leo tarehe 23 Disemba 2020. Kushoto ni Mama Florence Wamara, mke wa Nekemia kazimoto. Familia ya Mzee Nekemia Kazimoto ikiwa katika kaburi ya Mzee Nekemia Kazimoto baada ya ibada ya shukrani ikiwa ni mwaka mmoja baada ya kutwaliwa kwa Mzee Nekemia Musa Kazimoto, ibada hiyo imefanyika nyumbani kwake Omugakoroho, Kayanga Karagwe. Leo tarehe 23 Disemba 2020.
Picha Zote na Eliud Rwechungura
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment