JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAWASHIKILIA WATU SITA KWA TUHUMA ZA MAKOSA MBALIMBALI IKIWEMO MAUAJI | Tarimo Blog

 JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LILIMKAMATA  BENSON OLUOCHI, MIAKA 54, MLINZI, MKAZI WA MTAA WA CAPRIPOINT KWA TUHUMA ZA KUMUUA  MKE WAKE AITWAYE ELIZABETH BENSON, MIAKA 45, MSUKUMA, MJASILIAMALI, MKAZI WA CAPRIPOINT, CHANZO CHA TUJKIO HILI NI MTUHUMIWA KUMTUHUMU  MKEWE KUWA  HANA UAMINIFU KATIKA  NDOA ALIMSHAMBULIA KWA FIMBO  SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI NA BAADAE ALIPOTEZA MAISHA  MUDA  MFUPI WAKATI ALIPOFIKISHWA HOSPITALI YA MKOA SEKOU TOURE KWA MATIBABU. 

JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAKAMILISHA UCHUNGUZI NA MTUHUMIWA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI HARAKA IWEZEKANAVYO. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA MKOA SEKOU TOURE KWA UCHUNGUZI ZAIDI WA DAKTARI 


TUKIO LA PILI. VITA DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA 

TAREHE 20.12.2020 MAJIRA YA 17:12HRS HUKO MAENEO YA IGOMBE A, KATA YA BUGOGWA, WILAYA YA ILEMELA, MKOA WA MWANZA, JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LILIMKAMATA   SITTA GABUNGA, MIAKA 66, MKRISTO, MJITA, MKAZI WA IGOMBE, KWA KOSA LA KUPATIKANA NA DAWA ZA KULEVYA AINA YA BHANGI KIASI CHA GUNIA TANO NA MISOKOTO THELATHINI, IKIKADIRIWA KUWA NA UZITO WA KILOGRAMU 194, KITENDO AMBACHO NI KOSA LA JINAI. 

TUKIO LA TATU. MISAKO MIKALI KATIKATI YA JIJI NA WILAYA ZOTE.

JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAENDELEA NA  MISAKO MIKALI KATIKATI YA JIJI NA WILAYA ZOTE ZA MKOA WA MWANZA AMBAPO WATUHUMIWA SITA  WA WALIKAMATWA NA  VITU MBALIMBALI VYA WIZI.

WATUHUMIWA WALIOKAMATWA NI;-

  1. RAPHAEL SILI, MIAKA 25, MKAZI WA MAHINA, MWENDESHA PIKIPIKI (BODABODA)

  2. SEIFU SAID @RUBENGWA

  3. ISACK PETRO, MIAKA 34, MKAZI WA KISHIRI

  4. OSCAR PAUL, MIAKA 27, MKAZI WA IGOMA


VITU VILIVYOPATIKANA NI;-

  1. PIKIPIKI MOJA YENYE NAMBA MC 971 CDU AINA YA HONLG RANGI NYEKUNDU.

  2. TV FLAT SCREEN TATU MOJA AINA YA HISENSE, LG NA NYINGINE AINA YA LED.

  3. TV AINA YA LED FLAT SCREEN

  4. SOLAR AINA YA SUNDAR

  5. RADIO SUBWOOFER MBILI ZOTE AINA YA SEAPIANO.

 JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAENDELEA NA  MAHOJIANO YA KINA NA WATUHUMIWA PAMOJA NA MSAKO MKALI KATIKA MAENEO YOTE ILI KUWEZA KUBAINI NA KUWAKAMATA WATU WOTE WANAOJIHUSISHA NA VITENDO VYA KIUHALIFU. 

JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINATOA WITO KWA WANANCHI HUSUSANI WANANDOA/WATU WALIOKUA KWENYE MAHUSIANO KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI PINDI WANAPOKUA KWENYE MIGOGORO, BALI WAFUATE TARATIBU ZA KISHERIA NA KIDINI ILI WAWEZE KUSULUHISHWA KWA AMANI. VILEVILE LINAENDELEA KUTOA WITO KWA WANANCHI KUENDELEA KUTOA TAARIFA ZINAZOHUSU WAHALIFU NA UHALIFU ILI ZIFANYIWE KAZI KWA HARAKA NA WATUHUMIWA WAWEZE KUKAMATWA KABLA HAWAJATENDA MAKOSA . 

IMETOLEWA NA;

Muliro JUMANNE MULIRO - ACP

KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

22, DESEMBA 2020




Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2