JESHI LA ZIMAMOTO WATOA TAHADHARI KIPINDI CHA SIKUKUU YA KRISMAS | Tarimo Blog

 Na Mwandishi wetu, globu ya jamii

KUELEKEA msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka Jeshi la Zimamoto na uokoaji hapa ncini latoa tahadhari ili kusitokee matukio yatakayo athiri afya za wanajamii.

Jeshi hilo linajulisha umma kwa ujumla kuwa katika kipindi hiki cha Sikukuu za Krismas 2020 na Mwaka mpya 2021, litahakikisha maeneo yote yapo salama zikiwemo nyumba za ibada, fukwe na kumbi za starehe.

Katika Taarifa yake iliyotolewa na jeshi hilo imesema kuwa Wamiliki wa Kumbi za Starehe wahakikishe kuwa kumbi zao zimekaguliwa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na zimewekwa mifumo na vifaa vya kuzima moto, ili kuzuia majanga ya moto, kumbi ambazo hazitakidhi usalama hazitaruhusiwa kutumika.

"Wamiliki wa vyombo vya Usafiri na Usafirishaji na Madereva, pamoja na kuzingatia sheria zote za usalama barabarani, wanatakiwa kuwa na vizima moto kwenye magari yao." Imesema Taarifa hiyo.

Aidha Wazazi wanatakiwa kutowaacha Watoto wao na wenye mahitaji maalum peke yao, wanapokuwa kwenye matembezi bila ya kuwa na uangalizi wa karibu. Tunatoa rai kwa wananchi wanaotumia mapambo (Taa) ya krismas na mwaka mpya yanaweza kusababisha moto wachukue tahadhari ya hali ya juu.

Kwa huduma ya haraka juu ya majanga ya moto na maokozi Piga namba 114.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2