Na Khadija Self, Michuzi Tv
WAZAZI washauriwa kutowaficha watoto wenye magonjwa ya usonji.
Akizungumza hayo Jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Taasisi ya Lukiza Autism Hilda Nkabe amesema watoto wenye Matatizo ya Usonji wana haki za Kimsingi kama Watoto wengine.
"Watoto wenye usonji Mara nyingi wamekuwa wakifichwa na imejengeka imani potofu kuwa mtoto wa namna hiyo ni wakufungiwa ndani tu jamii inamtenga kuanzia michezo na mambo mengi ya kimsingi hapewi fursa yoyote ile." Amesema
Nkabe amesema Taasisi yake ikishirikiana na Miss Tanzania ambae ni balozi wa Taasisi ya Autism imeona ipo haja ya kukaribisha Sikukuu ya Christmass pamoja na Watoto wenye Usonji.
Aidha Kwa upande wake Miss Tanzania Rosemary Manfere amefurahi kujumuika na Watoto hao.
"Tumetazama Sinema pamoja pia Nimejifunza vingi kupitia watoto wenye Usonji na kutokana project yangu ilikua kuhusu watoto hao na imani sasa wazazi watakua karibu na Mimi ili tuweze kuwapata nafasi watoto hao kuonyesha uwezo wao mwengine sababu kuna watoto tofauti tofauti wenye usonji kuna watulivu ambao ukimwambia kitu anakuelewa,pia kuna yule hakusikii ila ukimpa ishara anakuelewa."
Pia Rosemary amewataka Wazazi kutowaficha watoto hao ili jamii iendelee kuelewa uwepo wa Watoto hao na haki zao za Kimsingi za Kuishi Kama Watoto Wengine.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment