KASI YA MIRADI YA DAWASA YAMKOSHA ASKOFU GWAJIMA | Tarimo Blog

 

Mbunge wa Jimbo la Kawe kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),  Askofu amefanya ziara ya kupata taarifa ya hali ya huduma na utekelezaji wa miradi ya majisafi katika jimbo la Kawe.

Katika ziara hiyo Askofu Gwajima ameridhishwa na kasi ya miradi ya maji inayoendelea kutekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) katika maeneo ya Makongo, Changanyikeni, Salasala, Mivumoni, Tegeta A, Mwabwepande, Mbopo na Kinondo Bunju ambapo ni sehemu ya jimbo la Kawe.

Askofu Gwajima amepongeza jitihada zinazofanywa na DAWASA ikiwemo utekelezaji wa mradi wa maboresho ya huduma ya maji kuanzia  Makongo hadi Bagamoyo uliohusisha ujenzi wa Matenki ya maji pamoja na pampu za kusukuma maji ambazo zitapelekea kuongeza upatikanaji wa maji wa wakazi wa jimbo la Kawe kwa sehemu zilizokuwa na changamoto ya huduma.

"Naiomba DAWASA kusimamia kwa karibu ujenzi wa tenki la maji lilipo eneo la Tegeta A litakalokuwa na ujazo wa Lita milioni tano ili kupunguza adha ya maji pamoja na migao ya mara kwa mara kwa wakazi wa Goba, Kinzudi, Kibururu, Matosa, Kulangwa  na Tegeta A inayotarajiwa kukamilika Oktoba 2021. alisema Askofu Gwajima 
Meneja wa DAWASA mkoa  wa Makongo Mhandisi Edison Robert Venance akitolea ufafanuzi kwa Mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima kuhusu Tanki la maji lililopo Changanyikeni wakati wa  ziara ya mbunge huyo iliyokuwa na lengo la kupata taarifa za utekelezaji wa Miradi ya maji katika jimbo hilo.
Meneja wa DAWASA mkoa wa Makongo Mhandisi Edison Robert Venance(kushoto) akitoa ufafanuzi kwa Mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima kuhusu kituo cha kusukumia maji eneo la Makongo Juu na kusambaza maji katika jiji la Dar es Salaam hasa kwenye jimbo la Kawe wakati wa Ziara yake ya utekelezaji wa Miradi ya maji katika jimbo hilo.
Muonekano wa kituo cha kusukuma maji (booster pump) eneo la Makongo Juu
Meneja Usambazaji kutoka DAWASA, Mhandisi Tyson Mkindi akionesha sehemu wanapohifadhia maji eneo la Chuo Kikuu mara baada ya kufika kwa ajili ya kuwekewa dawa pamoja na kusambaza maji kwenye maeneo mbalimbali ya jijini Dar es Salaam
Mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima akizungumza jambo wakati wa kutembelea kituo cha kusukuma maji (booster pump) eneo la Chuo Kikuu  wakati wa  ziara yake iliyokuwa na lengo la kupata taarifa za utekelezaji wa Miradi ya maji katika jimbo hilo.
Muonekano wa kituo cha kusukuma maji (booster pump) eneo la Chuo Kikuu
Meneja wa Mkoa waDAWASA Mivumoni Mhadisi Felchesm Kimaro akitoa ufafanuzi kwa Mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima kuhusu pampu inayosukuma maji katika tenki la maji la Salasala wakati wa Ziara ya kutembea miradi ya DAWASA iliyoko katika Jimbo la Kawe jijini Dar es Salaam
Mhandisi Eliud Simon kutoka DAWASA(wapili kulia) akijibu maswali yaliyokuwa yanaulizwa na Mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima pamoja na wananchi waliofika kwenye kituo cha kusukuma maji (booster pump) eneo la Salasala wakati wa ziara yake iliyokuwa na lengo la kupata taarifa za utekelezaji wa Miradi ya maji katika jimbo hilo.
Muonekano wa kituo cha kusukuma maji (booster pump) eneo la Salasala
Meneja wa DAWASA mkoa wa Mivumoni Mhandisi Felchesm Kimaro(wa kwanza kushoto) akitoa taarifa ya mradi wa Tanki la maji la Salasala kwa Mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima wakati wa  ziara yake iliyokuwa na lengo la kupata taarifa za utekelezaji wa Miradi ya maji katika jimbo hilo.
Meneja wa DAWASA mkoa wa Mivumoni Mhandisi Felchesm Kimaro(kulia) akionesha sehemu moja inayoweza kufungwa wakati sehemu nyingine maji yanasambazwa kwa ajili ya kufanyia usafi eneo hilo wakati wa ziara ya Mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima ili kupata taarifa ya miradi mbalimbali inayosiamiwa na DAWASA.
Meneja wa DAWASA mkoa  wa Mabwepande, Haruna Taratibu(kulia) akitoa taarifa kwa Mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima (kushoto) kuhusu mradi wa ujenzi wa Tanki la kuhifadhia maji la Mabwepande la kuhifadhia maji namna litakavyoweza kuhudumia mitaa mbalimbali ya katika Jimbo la Kawe lililopo jijini Dar es Salaam.
Meneja wa DAWASA mkoa  wa Kawe,  Judith Singinika(wa pili kulia) akitolea ufafanuzi maswali aliyokuwa anauliza  Mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima kuhusu miradi maji inayoendeshwa na kusimamiwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA).
Mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima(wa pili kushoto) akizungumza na wakandarasi wa ujenzi wa Tanki la kuhifadhia maji katika eneo la Tegeta A unaotekelezwa chini ya mradi wa usambazaji maji Makongo – Bagamoyo wakati wa ziara yake iliyokuwa na lengo la kupata taarifa za utekelezaji wa Miradi ya maji katika jimbo hilo.
Muonekano wa Sehemu itakayojengwa Tanki la kuhifadhia maji katika eneo la Tegeta A 
Mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima(wa pili kulia)  akitoa mjumuhisho wa mara baada ya kumaliza ziara kupata taarifa za utekelezaji wa Miradi ya maji katika jimbo hilo.

Picha za pamoja

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2