WANANCHI wanaopata huduma ya afya katika hospital ya Turiani wilayani Mvomero wamesema huduma wanazopata katika hospitali hiyo ziko juu na kusababisha baadhi ya wananchi kushindwa kumudu gharama za matibabu.
Wamesema kuwa wanashukuru ziara ya mbunge kufanya katika hospitali hiyo huku wakisema gharama zilizopo zingepunguzwa kutokana na hali za maisha ya watu.
Wananchi wameyasema hayo wakati wa ziara ya mbunge wa Jimbo la Mvomero Jonas Van Zeeland.
Zeeland baada ya kuwajulia hali Wagonjwa amesema kuwa ataangalia namna kuishauri serikali namna ya kuwapunguzia gharama ili wapate matibabu tofauti na ilivyo sasa ikiwemo kuchelewa kupata huduma wawapo hospitalini.
Katika ziara hiyo ametembelea katika wodi za wagonjwa na kuzungumza nao ikiwa ni pamoja ya kuwatia faraja zaidi.
Zeeland amesema atayafikisha changamoto hizo kwenye ngazi husika huku baadhi ya watumishi wakimueleza mbunge kuwa kwa kipindi cha miezi mitano hawajalipwa mishahara yao kutokana na hospitali kutegemea chanzo kimoja cha mapato ambacho ni fedha zinazotolewa na wagonjwa, hali ambayo imesababisha kukosekana kwa fedha za kulipa mishahara baada ya wagonjwa kupungua hospitalini hapo
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment