*Waajiri waahidi kuchukua Wahitimu katika fani mbalimbali kutoka VETA.
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
WAHITIMU wa vyuo vya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) ni muhimu katika kusukuma Maendeleo ya viwanda nchini, Serikali ya awamu ya tano imekwenda na kauli mbiu ya viwanda ambapo mafundi na wajuzi watazalishwa katika vyuo vya VETA kwa ajili ya kutumikia viwanda hivyo.
Hayo aliyasema Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Temeke Deogratius Lukomanya wakati wa Mahafali ya 50 ya Chuo cha VETA Chang'ombe katika mahafali ya 50 yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Lukomanya amesema vijana waliohitimu wasibweteke kwa kutegemea ajira kwani kuwa mafunzo ya ufundi Stadi ni ajira ya uhakika kinachotakiwa ni ubunifu na kujua soko linaendaje.
Amesema katika vitu alivyoviona katika Chuo Cha VETA Chang'ombe hakutegemea umahiri wa vitu wanavyovifanya huku akiwaasa vijana kujituma zaidi pamoja na kuanzisha vikundi na kuzalisha bidhaa na kuingiza sokoni na kuweza kupata mafanikio kwao binafsi pamoja na nchi kwa ujumla.
Lukomanya amesema wahitimu waondokane na dhana ya kuletewa ajira bali wajitume kwa kujitengenezea ajira zao kutokana mafunzo ya VETA.
"Katika karne hii ya 21 upatikanaji wa ajira umekuwa ni changamoto kubwa Duniani hivyo wajibu kuwa na mawazo ya kujitengenezea ajira wenyewe kwa ujuzi mliopata".amesema Lukomanya.
Amesema wahitimu waendelee kuwa waminifu na moyo wa kufanya kazi kwa kujituma katika sehemu zao kazi ili waweze kupata mafanikio.
Aidha amewaomba waajiri kuendelea kupokea vijana na kuwapatia nafasi za mafunzo kwa vitendo viwandani pamoja na nafasi za ajira kwa vijana pale zitakapopatikana.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo VETA Chang'ombe Joseph Mwanda amesema kuwa mwaka huu 2020 Chuo kimeweza kusajili jumla ya wanafunzi 1,361 wa mwaka wa kwanza, wa pili na wa tatu kwa kozi za muda mrefu na diploma ya ubunifu wa mitindo ya mavazi.
Amesema Chuo hicho kina wanafunzi wenye mahitaji maalumu ikiwa ni pamoja na watu wenye ulemavu wa mfumo wa fahamu na watu wenye ulemavu wa viungo ambapo wengi wao wameonyesha uwezo mkubwa kwenye mafunzo yao wa kuweza kufanya vitu tofauti katika jamii.
"Mwaka 2020 tuna wanafunzi wenye mahitaji maalumu 21 katika fani mbalimbali. Kati yao wanafunzi 10 ni wenye ulemavu wa mfumo wa akili na wanafunzi 11 ni wenye ulemavu wa viungo."Amesema Mwanda.
Mwanda amesema changamoto kubwa ambazo wanakumbana nazo ni pamoja na uhaba wa majengo na samani kwaajili ya wanafunzi wa kozi ndefu na fupi kwa karibu nusu ya mahitaji.
Akizungumza kwa niaba ya wazazi wote Avelina Mrema amewahimiza wahitimu kutokata tamaa katika maisha yao kwani ndio ukurasa mpya umefunguliwa na kutokana na mafunzo
Pia Mkurugenzi wa Kampuni ya Reverse pamoja na kampuni wamekubaliana kuchukua wahitimu katika fani mbalimbali.
Amesema kuwa wahitimu wa VETA wameiva katika mafunzo hivyo wana uhakika wanaweza kufanya vitu vya ziada sehemu zao za kazi.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment