MUHAS WAMPONGEZA DKT MWAKYEMBE KWA KUTEULIWA MWENYEKITI WA BARAZA LA CHUO HICHO | Tarimo Blog


Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv

CHUO Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS)  kimempongeza Dkt Harrison Mwakyembe kwa kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la chuo hicho.


Pongezi hizo zimetolewa wakati wa mahafali ya kumi na nne (14) tangu Chuo cha MUHAS kiwe Chuo Kikuu kamili mwaka 2007.

Akizungumza wakati wa mahafali hiyo, Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Andrea Pembe amesema kuchaguliwa kwa Dkt Mwakyembe wanamuhakikishia ushirikiano mzuri na karibu sana kwa maendeleo ya Chuo na taifa kwa ujumla.

Aidha, Prof Pembe wamemshukuru Mwenyekiti wa Baraza la Chuo aliyemaliza muda wake Mariam Mwaffisi kwa juhudi na utendaji wake wa kazi uliotukuka katika kipindi chote ambacho alihudumu kwenye nafasi hiyo ndani ya baraza la chuo na kukisaidia pindi changamoto zinapotokea na kuweza kufikia hapa walipo.

Dkt Mwakyembe mapema wiki iliyopita aliteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha MUHAS akichukua nafasi ya Mariam Mwaffisi aliyemaliza muda wake.
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi  Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Dkt Harrison Mwakyembe akizungumza wakati wa mahafali ya 14 ya Chuo hicho yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.



Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2