NIC YATOA VITABU VYENYE THAMANI YA MIL. 3 KWA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU. | Tarimo Blog

 

NA MWANDISHI WETU.

SHIRIKA la Bima la Taifa (NIC) limelenga kutoa  vitabu vya maswala ya Ukimwi kwenye vyuo vya elimu ya juu vinavyogharimu shilingi milioni 3 za kitanzania kwa lengo la kuwaelimisha juu ya ugonjwa huo  kuepukana na maambukizi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa kupokea vitabu hivyo , Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja wa Shirika hilo Bw. Yessaya Mwakifulefule amesema kuwa NIC  imenunua vitabu hivyo ili kuvisambaza kwenye vyuo vya elimu ya juu ili kutoa elimu kwa vijana namna ya kupambana na ugonjwa huo.

“Tumeamua kurudisha kwa jamii kile tunachokipata kwa kupeleka vitabu vinavyotoa elimu ya ukimwi kwa wanafunzi wa vyuo vikuu ili kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli”  alisema Mwakifulefule.

Aidha Mwakifulefule amesema kuwa NIC imenunua vitabu hivyo  kutoka Book Aid ili kuongeza chachu ya kukua kwa uchumi wa kati kupitia viwanda ili kukuza biashara na taaluma za watanzania katika kutoa elimu kwa jamii.

Kwa upande wake  mtunzi wa kitabu hicho Dkt. Elizabeth Mwanukuzi amesema nchi za Afrika kusini mwa jangwa la Sahara zimeathirika Sana na ugonjwa wa ukimwi hicho aliona ni vyema akaandika kitabu hicho ili kusaidia nchi katika kutoa Elimu ya  mapambano dhidi ya  ukimwi hasa katika vyuo vikuu vyetu kwa sababu Hawa ndiyo nguvukazi ya taifa wakati ujao.

Dk.Mwanukuzi ameongeza kuwa mbali kutoa Elimu ya  kujikinga na ukimwi kwa wanafunzi wa vyuo vyetu  watanzania wajiwekee utaratibu wa kuwa na bima za maisha pamoja na mali zao kutoka Shirika la Bima la taifa NIC  kwa manufa yao ya baadae.

“ Vijana kama Bodaboda na wengineo wanatakiwa kukata bima za vyombo vyao vya moto ili kuwaondolea usumbufu pale wanapopata ajali au wanapoharibikiwa vyombo vyao vya moto “ alisema Dkt. Mwanukuzi.

Shirika la Bima la taifa NIC ni shirika linalotoa huduma za bima ikiwemo Bima ya maisha, Bima ya elimu, Bima ya vyombo vya moto kama vile magari na pikipiki pamoja na Bima za moto pale nyumba yako inapopata majanga ya moto na mafuriko au matetemeko ya ardhi.

Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja Shirika la Bima la taifa NIC Bw.Yessaya Mwakifulefule akipokea kitabu kinachoelemisha wanafunzi wa vyuo vikuu katika masuala ya mapambano ya ukimwi kutoka kwa Mwandishi wa kitabu hicho Dkt.Elizabeth Mwanukuzi kutoka kampuni ya Book Aid baada ya Shirika Hilo kutoa udhamini wa vitabu hicho kwa ajili ya wanafunzi

Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja Shirika la Bima la taifa NIC Bw.Yessaya Mwakifulefule akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 3 kwa Dk. Elizabeth Mwanukuzi kutoka kampuni ya Book Aid kwa ajili ya udhamini wa kitabu kinachoelemisha wanafunzi wa vyuo vikuu katika masuala ya mapambano ya ukimwi baada ya Shirika Hilo kutoa udhamini wa vitabu hivyo kwa ajili ya wanafunzi
 



Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2