Rais Uhuru Kenyatta ahudhuria mkutano wa Jumuiya ya IGAD | Tarimo Blog

 

Rais Uhuru Kenyatta na viongozi wengine wamehudhuria mkutano wa 38 wa viongozi wa mataifa ya jumuiya ya (IGAD) ambao umefanyika Djibouti.

Mkutano huo uliongozwa na waziri mkuu Abdalla Hamdok wa Sudan ambaye ni mwenyekiti wa mkutano wa IGAD na kuhudhuriwa na rais Ismail Omar Guelleh (Djibouti), Mohamed Abdullahi (Somalia) na waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed

Katika mkutano huo ambao ulihudhuriwa pia na mwenyekiti wa tume ya umoja wa Afrika-African Union Commission (AUC) Moussa Faki Mahamat, makamu wa rais wa Sudan Kusini na Uganda Rebecca Garang na Amb Rebecca Otengo.

Katika utangulizi ,mwenyeji wa mkutano huo rais Ismail Guelleh alipongeza jitihada zinazofanyika katika kutafuta amani na utulivu katika ukanda huo licha ya janga la corona na changamoto nyingine za mafuriko pamoja na jangwa la ukame lililosababishwa na uvamizi wa nzige.

Katika hotuba yake, mwenyekiti wa AUC bwana Moussa Faki Mahamat alisema mvutano wa kidiplomasia kati ya Kenya na Somalia ni suala ambalo Umoja wa Afrika una wasiwasi nao.

Bwana Mahamat aliitisha mazungumzo haya ili mvutano huo wa mataifa majirani ambayo yana historia ya uhusiano mzuri kwa muda mrefu , kwa mfano Kenya imejitoa pakubwa kutoa wanajeshi wake katika jumuiya ya Afrika nchini Somalia (AMISOM) na kusaidia kupokea wakimbizi wengi wa Somalia .

Kwa upande wa Ethiopia,mwenyekiti wa AUC iliwataka wanachama wa IGAD kusaidia taifa hilo kwa misaada ya kibinadamu kufuatia ghasia zilizokuepo Tigray.

Waziri mkuu Hamdok alisema mkutano huo uliitishwa ili kujadili masuala mbalimbali ya amani katika ukanda huo katika upande wa amani na usalama wa Sudan, Sudan Kusini , Ethiopia na Somalia.

Rais Kenyatta, ambaye aliwasili Djibouti Jumapili asubuhi aliongozana na waziri wa mambo ya nje Raychelle Omamo.

 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2