SERIKALI KUSHUSHA RUNGU KWA WAKOPESHAJI UMIZA WA PEMBEJEO KWA WAKULIMA | Tarimo Blog


Nolasco Kilumile afisa wa mazao kutoka halmashauri ya mji wa Njombe (HQ) akifafanua namna halmashauri itakavyoendelea kupambana na wakopeshaji umiza wa pembejeo za kilimo kwa wakulima pamoja kuwataka wakulima kujenga mitaji yao wenyewe kuliko kutegemea mikopo zaidi.
Bethseba Betty Liduke mkurugenzi wa shirika la Highlands hope Umbrella (HHU) akiwaeleza namna mradi unavyofanya kazi ya kilimo ,wataalamu wa kilimo pamoja na wajumbe wengeine wakiwemo madiwani katika warsha ya mrejesho wa mradi wa kilimo unaotekelezwa kwenye tarafa ya Igominyi Halmashauri ya mji wa Njombe.
Baadhi ya wajumbe waliofika kwenye washa ya kupata mrejesho wa utekelezaji wa mradi wa kilimo wakisikiliza namna wakulima watakavyofanikiwa kufikiwa na shirika la HHU katika utekelezaji wa kilimo bora.


Na Amiri Kilagalila,Njombe

HALMASHAURI ya mji wa Njombe imejipanga kupambana na mashirika ya kilimo yanayotoa mikopo kandamizi ya pembejeo kwa wakulima kwa mgongo wa kutoa misaada yakiwa kwa kivuli cha NG’O wakati ni makampuni ya kibiashara yanayotafuta faida.

Serikali imejipanga kuendelea kufuatilia mashirika hayo kutokana na malalamiko kutoka kwa wakulima kuingia kwenye migogoro na mashirika hayo baada ya kushindwa kurejesha mikopo kutokana na ulaghai unaofanywa na baadhi ya mashirika pamoja na wakulima wengine kushindwa kufikia malengo ya uzalishaji wakati wa mavuno.

Onesmo Kamonga ni afisa ugani wa kata ya Iwungilo na Suzana Kiwele ni afisa kilimo wa kata ya Kifanya kwa niaba ya wakulima,wakizungumza katika kikao cha mrejesho wa mradi wa kilimo kutoka shirika la Highlands hope Umbrella (HHU) unaotekelezwa katika tarafa ya Igominyi Njombe mjini,wamesema wamekuwa wakipokea malalamiko kutoka kwa wakulima wakilubuniwa pembejeo kwa kukopeshwa kwa bei naafuu ili hali wakati wa mavuno wamekuwa wakilipa zaidi ya makubaliano.

“Mkulima anapenda sana afanikiwe kwa hiyo wakiona shirika linatoa labda mbolea hawezi kuacha sasa tunapata malalamiko kwa kuwa awali mashirika yanakuja kwa lugha tamu ila mwisho wa siku baada ya mavuno liba yake inakuwa ni kubwa tofauti na walichokipata”alisema Suzana Kiwele

“Ili kuondoa malalamiko ya mara kwa mara mimi niwaombe wakulima wajenge msingi wa kujitegemea kuliko kuendesha kilimo kwa mikopo kwa kila kitu na wakopeshaji wengine wako kibiashara zaidi”alisema Onesmo Kamonga

Bethseba  Liduke ni mkurugenzi wa shirika la Highlands hope Umbrella (HHU) amesema kwa sasa wameingia katika kilimo ili kuongeza nguvu ya mabadiriko ya kilimo bora ufanisi na chenye tija mkoani Njombe,huku akiwashauri wakulima kuwa makini na mashirika yanayofika kwenye maeneo yao,pamoja na serikali kuendelea kupambana na mashirika umiza.

“Niwashauri wakulima wawe makini na haya mashirika yanayoingia kwenye maeneo yao,na tuombe sana serikali iweze kuingilia kati na kuwasaidia wakulima wanapongia kwenye migogoro na mashirika”alisema Beth Liduke

Bi,Liduke aliongeza “Safari hii tumeingia kwenye kilimo kwasababu kwa Njombe ni uti wa mgongo lakini wakulima wamekuwa na kilimo cha mazoea,na tunachohitaji watu walime kilimo bora chenye ufanisi na kitakacholeta matokeo chanya kwa mkulima”aliongeza Bi,Liduke

Nolasco Kilumile ni afisa wa mazao kutoka halmashauri ya mji wa Njombe (HQ).Amesema mashirika mengi yanakuja kwa mgongo wa NG’O  lakini wanafanya biashara hivyo amewataka wakulima kukopa kwa hiari yao huku akiwataka kujenga mitaji yao wenyewe.

Vile vile amesema wanaendelea kuyafuatilia mashirika yanayofanya kazi kwa mwamvuli wa NG’O wakati yanatafuta faida kwa kutoa mikopo mibaya na ya kuumiza wakulima.

“Haya mashirika tunaendelea kuyafuatilia,yale yenye mikopo mibaya lazima tuyafutilie kama tulivyofanya kwa moja ya shirika siwezi kulitaja hapa,lazima tuhoji kwa mwamvuli wa NG’O inakuwaje wewe utafute faida”alisema Nolasco.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2