Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu kutoka Wizara ya Afya- Idara Kuu
ya Maendeleo ya Jamii Mathias Haule akisisitiza jambo wakati
Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Mtoto kutoka Wizara ya Afya- Idara
Kuu ya Maendeleo ya Jamii Mwajuma Magwiza (mwenye Hijab) akiwa na timu ya wataalam kutoka Wizara hiyo na TAMISEMI wakiangalia mradi wa ujenzi wa Kituo cha Malezi ya watoto wadogo kinachoshirikisha Jamii, Serikali
na Shirika la Brac kilichopo katika Shule ya Msingi Mbutu katika
Manispaa ya Kigamboni jijini Dar Es Salaam.
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa Kituo cha Malezi kwa Watoto
katika Shule ya Msingi Mbagala Kuu, Manispaa ya Temeke chenye lengo la
kutoa Malezi kwa watoto pale wazazi wanapokuwa katika majukumu ya
kutafuta riziki Vituo hivi vinashirikisha nguvu za wananchi, Serikali
na Shirika la Brac na vituo 30 katika mikoa ya Dodoma na Dar Es Salaam
vinaendelea kujengwa katika maeneo tofauti.
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu kutoka Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Mathias Haule akisisitiza jambo wakati Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Mtoto kutoka Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Mwajuma Magwiza (mwenye Hijab) akiwa na timu ya wataalam kutoka Wizara hiyo na TAMISEMI wakiangalia mradi wa ujenzi wa Kituo cha Malezi ya watoto wadogo kinachoshirikisha Jamii, Serikali na Shirika la Brac kilichopo katika Shule ya Msingi Mbutu katika Manispaa ya Kigamboni jijini Dar Es Salaam.
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii kwa kushirikiana na Shirika la Brac Tanzania imeanza kuratibu uanzishwaji wa Vituo vya Malezi kwa watoto wadogo vitakavyomilikiwa na kuendeshwa na Jamii ya eneo husika.
Hayo yamesemwa jijini Dar E s Salaam na Mkurugenzi wa Idara ya
Maendeleo ya Mtoto kutoka Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya
Jamii Mwajuma Magwiza wakati akikagua Maendeleo ya uanzishwaji wa
vituo hivyo kwa Halmashauri za Wilaya ya Temeke na Kigamboni
vinavyojengwa kwa ushirikiano wa Wananchi, Serikali na Shirika la
Brac.
Bi. Mwajuma amesema lengo la uanzishwaji wa Vituo vya Malezi kwa
watoto katika kijamii ni kuhakikisha watoto wanapata sehemu sahihi ya
kukaa na kulelewa wakati wazazi na walezi wanapokuwa katika majukumu
ya kutafuta riziki.
Ameongeza kuwa vituo hivyo vya Malezi pia vitasaidia kuondokana na
vitendo vya Ukatili kwa watoto wadogo ikizingatiwa kuwa watoto hao
hufanyiwa vitendo vya Ukatili katika jamii zetu.
" Vituo hivi vitakuwa chini ya jamii husika na vitasaidia malezi kwa
watoto pale wazazi na walezi wanapokuwa katika majukumu ya utafutaji
wa kipato." alisema.
Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Mbagala Kuu Fabian Chilumba amesema kuwa
wameupokea mradi huo kwa dhati na atahakikisha anahamasisha wananchi
waendelee kuchangia nguvu zao kuhakikisha mradi inaisha kwa wakati na
kuanza kutumika.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Somangila na Naibu Meya Manispaa ya
Kigamboni Mhe. Steven Warioba amesema kuwa kuna uhitaji mkubwa wa
vituo hivyo katika Mitaa kwani kuna watoto wengi wanahitaji huduma ya
uangalizi wakati wazazi hawapo nyumbani.
Naye Diwani Kata ya Kimbiji Muhidini Budaya amesema atashirikiana na
viongozi wa Manispaa ya Kigamboni kuhamasisha wananchi kushiriki
katika ujenzi wa vituo hivyo ili kuhakikisha watoto wao wanapata
sehemu sahihi ya kulelewa wakati wakiwa katika majukumu ya kutafuta
riziki.
Aidha Meneja Mradi kutoka Shirika la Brac, Novatus Tarimo amesema
Shirika lao linashirikiana na wananchi katika kuhakikisha mradi wa
ujenzi wa Vituo hivyo vya Malezi kea Watoto kwa ngazi ya Jamii
inakamilika na inaaza kutumiwa na Watoto wa Jamii husika.
Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Brac na wananchi kuchangia
nguvu zao inaendesha zoezi la ujenzi wa mradi wa Vituo vya Malezi kwa
Watoto wadogo kwenye ngazi ya Jamii katika mikoa ya Dodoma na Dar Es
Salaam ambapo, jumla ya Vituo 30 vinajengwa katika Mitaa ya
Halmashauri mbalimbali za mikoa hiyo.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment