Na Nathaniel Limu, Singida
KANISA la Pentekoste (FPCT) mjini kati Singida,limemshukru na
kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Magufuli kwa
ujasiri wake wa kuwaaminisha Watanzania kwamba mbele ya Mungu ugonjwa hatari wa corona hautaisumbua nchi.
Shukurani na pongezi hizo zimetolewa jana (25/12/2020) na askofu
mstaafu Dk.Paulo Samwel, muda mfupi kabla ya kumkaribisha mhubiri wa
kimataifa bishop Dk.CJ Machibya kutoa mahubiri kuhusu maadhimisho ya siku ya kuzaliwa Yesu Kristo.
Dk. Samwel alisema mapema Rais Magufuli aliagiza kila mtanzania kwa
imani yake ya dini,afunge siku tatu mfululizo, kumwomba Mungu aiepushe
Tanzania na kusambaa kwa virus vya COVID 19. Mungu alisikiliza maombi
hayo.
“Rais wetu Dk.Magufuli kipenzi cha wanyonge amejipambanua kwamba
anaamini mbele ya Mungu,hakuna lisilo wezekana.Kutokana na ukweli
huo,chini ya uongozi wake miradi mingi na mikubwa imetekelezwa kwa
kipindi kifupi cha miaka mitano.Watanzania walio wengi hawakuamini
kama miradi hiyo ingetekelezeka.Lakini imetekelezeka”,alisema.
Hata hivyo, Dk.Samwel ametoa tahadhari kwa Watanzania kwamba
wasibweteke wakaacha kuendelea kumwomba Mungu aiepushe Tanzania na
ugonjwa corona.Waendelee kumwomba Mungu ili Watanzania waendelee
kuchapa kazi halali.
Katika hatua nyingine,askofu mstaafu ,amelipongeza jeshi la polisi
mkoa wa Singida, kwa kazi nzuri ya kuhakikisha amani na utulivu
unaendelea kudumishwa kipindi hiki za kusherehekea siku kuu za
kirismas na mwaka mpya.
“Polisi wetu wa manispaa ya Singida wapo vizuri.Usiku wa kuamkia leo, kanisani kwetu baadhi ya waumini wamekesha kwa ajili ya
kuadhimisha kuzaliwa kwake Yesu kristo.Shughuli hiyo wamedumisha
amani na utulivu mkubwa. Baadhi ya askari polisi wamefanya doria usiku
kucha kuhakikisha pamoja na mambo mengine,waumini wa dini
hawabughuziwi”,alisema.
Aidha,Dk.Samwel alisema siku hii leo ya ijumaa,ni siku ya maombi kwa
waumini wa dhehebu la kiislamu na kikiristo.Kwa hiyo ni siku maalum
Mungu ameitoa.
Kabla muhubiri wa kimataifa Bishop Dk.Machibya,hajaanza kutoa mahubiri
yake juu ya kuzaliwa kwa Yesu kristo,aliongoza wimbo wa kuzaliwa kwa
Yesu (Happy to you,Happy to Jesus and happy to chrismas).
Baada ya wimbo huo,Dk Machibya amewataka Watanzania kuishi kwa uasilia
wao waliopewa na Mungu,na wala wasithubutu kumkosoa Mungu kwa uumbaji
wake.
Alisema utakuta mwanamke ananyoa nyusi za juu ya jicho na kuweka kitu
kipya ambacho mbele ya safari kitendo hicho kigeni,kinaleta madhara na
mateso makubwa kwa mhusika.
“Wewe ishi kwa uhalisia wako…Mungu alivyokuumba,baki hivyo hivyo.Hizi
nywele juu ya jicho,usizitoe ukizitoa utakuwa unakosoa kazi ya
Mungu.Utapata shida.Nikuombe tu hizo nywele au sehemu yo yote mwili
iliyoumbwa na Mungu,usitoe cho chote.Wewe boresha tu.Rangi yako nyeusi
acha ibaki vile vile.Tofauti na hivyo,utajitafutia matatizo ikiwemo
kudhuruka kwa mwili”,amesisitiza mhubiri huyo wa kimataifa.
Aidha,amewataka Watanzania kujenga utamaduni wa kutoa zawadi kwa
rafiki na watu wote wenye mahitaji maalum.
“Huku kwetu barani afrika mambo ya kutoa zawadi kwa binadamu
mwenzake,ni issue.Ulaya ni jambo la kawaida watu kupeana zawadi hasa
vipindi vya siku kuu.Ulaya hata watu wenye tatizo la afya ya
akili,wanatoa zawadi.Kwetu sisi wenye nywele ngumu,na sisi tupo vivyo
vivyo wagumu kutoa zawadi.Naomba tubadilike utamaduni wa kupeana
zawadi,unaimarisha mahusiano mema”,amesisitiza.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment