Kampuni ya simu inayoongoza kidijitali nchini, Vodacom Tanzania PLC, inaendelea kuongeza thamani halisi kwa wateja, raia na nchi kwa ujumla., ambapo kipindi hiki cha sikukuu inatoa gawio la jumla ya TZS 3,928,312, 789 kwa wateja wake wa M-Pesa. Malipo ya gawio hili ni ya robo ya kwanza ya mwaka wa fedha wa kampuni hiyo (Aprili hadi Juni 2020).
Akizungumza na waandishi wa habari leo, kwa niaba ya Mkurugenzi wa M-Pesa, Epimack Mbeteni, Mkuu wa Idara ya M-Pesa Biashara Happiness Shuma alisema M-Pesa imekuwa ikija na masuluhisho mapya yenye ubunifu wa hali ya juu ambayo yamesababisha kuongezeka kwa thamani kwa wateja, idadi ya watumiaji na mapato ambayo yananufaisha kila mtu.
"Katika mwaka wa fedha uliopita, Vodacom ilirekodi ukuaji wa mapato ya huduma, ambayo kwa kiasi kikubwa ilisababishwa na ongezeko la matumizi ya huduma ya M-Pesa. Mapato ya M-Pesa yalikua kwa 7.4%, ikichangia TZS 358.2 bilioni kwa jumla ya mapato,” alisema Shuma.
Mtandao huu wenye kasi zaidi nchini unajivunia matokeo chanya ambayo umekuwa ukileta kwa wateja wake pamoja na uchumi wa nchi kwa jumla katika kuongeza matumizi ya kidijitali kupitia mabadiliko ya mfumo wa ikolojia ya malipo na kubadilisha maisha ya mamilioni ya Watanzania kupitia teknolojia pamoja na kutengeneza ajira zisizo za moja kwa moja kwa zaidi ya Watanzania 135,000.
"Tutaendelea kuongoza katika ubunifu, ili kuleta Watanzania wengi katika huduma jumuishi za kifedha, kuongeza idadi ya wateja wanaotumia huduma za M-Pesa pamoja na kupanua huduma zetu za biashara, tukizingatia ushirikiano wa kimkakati na kudumisha aina anuwai za huduma zinazofanya malipo kuwa ya haraka , rahisi na salama zaidi kwa wafanyabiashara na watu binafsi,” alihitimisha Shuma.
Ili kuweza kufahamu kiasi ambacho mteja wa M-Pesa atapokea, unashauriwa kuingia sehemu ya ujumbe mfupi, andika neno KIASI au AMOUNT halafu tuma kwenda namba 15300, utapokea ujumbe mfupi wenye kiasi ambacho mteja wetu wa M-Pesa utapokea kama gawio lako.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment