Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uwekezaji) Prof. Kitila Mkumbo wakati akizungumza katika mkutano Mkuu wa Mwaka wa Majalisi Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Siku ya Alhamisi tarehe 17 Desemba 2020 ambao umeambatana na utoaji wa zawadi kwa wanafunzi wahitimu 211 ambao wamefanya vizuri katika masomo yao.
Prof. Mkumbo amesema kwa sasa nchi inahitaji vijana wabunifu na wazalendo ambao watakuwa chachu katika kuwekeza katika miradi mbalimbali ikiwemo ya kilimo ,ufugaji, na uvuvi huku akiweka msisitizo kwa vyuo vikuu nchini kuwa na utaratibu wa kuwaandaa vijana katika kuwafundisha zaidi namna ya kujiajiri pasipo kusubiri ajira kutoka serikalini. “Lazima tubadilike kwenye ufundishaji wetu na tujue wanafunzi wanasoma nini ,kwa sasa dunia imebadilika tunahitaji vijana wanaoweza kujiajiri kwa hiyo sisi kama taasisi inayotoa elimu lazima tuwaandae vijana wetu zaidi kwenye kwenda kujiajiri, tukiweza kufanya hivyo na vijana wetu wakaelewa basi taifa letu litaondokana na changamoto ya ukosefu wa ajira” alisema Prof. Kitila Mkumbo.
Kwa upande wake Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo upande wa Taaluma Prof. Maulid Mwatawala amesema SUA ni miongoni mwa vyuo ambavyo vinawaandaa wanafunzi zaidi kwenye kujiajiri na kusema kuwa SUA itakuwa mfano wa kuigwa nchini.“Mhe. Waziri nikuakikishie tuko vizuri, wanafunzi wote wanaosoma masuala ya kilimo, mifugo, uvuvi na masuala ya utalii hawa wote tunawaandaa ili waweze kujiajiri”alisema Prof. Maulid Mwatawala
Katika mkutano Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais (Uwekezaji) Prof.Kitila Mkumbo amemkabidhi mwanafunzi Musa Gese Doto tuzo mbili tuzo ya Mbunifu Bora wa Teknolojia ambapo amebuni gari shamba tuzo ambayo imetolewa na SETO TV na tuzo ya mbunifu bora wa Mwaka 2020 ambayo imetolewa na Tanzania Universities and Colleges Students Awards.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment