Wanawake wa Manispaa ya Kigamboni wakiwa katika picha ya Pamoja Taasisi ya Internet Sociaty Tanzania mara baada mafunzo.
Afisa Maendeleo ya Jamii na Mratibu wa Dawati la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Tanzania Masesa Luanda akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo kwa wanawake wa Manispaa ya kigamboni wanaotumia mitandao ya kijamii katika biashara.
Nazar Kirama wa Internet Sociaty Tanzania akitoa mafunzo kwa wanawake namna ya kutumia mitandao ya kijamii kuendesha biashara kwa wanawake wanaofanya biashara kwa kutumia mitandao ya kijamii.
IMEELEZWA kuwa matumizi ya mitandao ya Internet yanakuwa kasi na yametoa fursa biashara kupitia kutumia mitandao mbalimbali ya kijamii.
Hayo aliyasema Nazar Kirama wa Internet Sociaty Tanzania wakati akitoa mafunzo kwa wanawake wa Manispaa ya Kigamboni jijini Dar es Salaam, Kirama amesema kuwa wanawake wengi wanafanya biashara kwa kutumia mitandao hivyo wanahitaji kupata mafunzo pia katika utumiaji wa mawasiliano salama.
Amesema kuwa katika utumiaji wa mitandao kuna watu wanatumia mitandao ya simu kwa ajili ya kufanya utapeli ambapo wafanyabiashara hiyo wanatakiwa kuwa na umakini.
"Tunahitaji mawasiliano yatumike kwa usalama na kufanya biashara ziweze kuendelea kwani serikali imeimarisha huduma za mawasiliano na kutoa fursa za biashara katika mitandao"amesema Kirama.
Hata hivyo amesema kuwa kuwa mafunzo hayo wameyatoa kwa katika makundi mbalimbali ya wanawake wanaofanya biashara ili ziweze kuwa salama.
Naye Mgeni rasmi katika mafunzo ya wanawake ya utumiaji wa Internet na mitandao ya kijamii Afisa Maendeleo ya Jamii na Mratibu wa Dawati la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Masesa Luanda amesema wanawake wanaweza kufikisha uchumi kuwa juu.
Luanda amesema kuwa wanawake katika uchumi kati tunahitaji kuchangamkia fursa za biashara hata kununua bidhaa nje ya nchi bila ya kwenda.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment