Na Jane Edward, Michuzi TV Arusha
Waziri wa Nishati Dkt.Medard Kalemani ametoa miezi mitatu hadi kufikia machi 31 mwakani kwa mkandarasi wa mradi wa kituo cha kupoozea umeme cha Lemugur kata ya Mateves mkoani Arusha kuhakikisha unakamilika ndani ya miezi mitatu kwani upo nje ya wakati.
Waziri ametoa maagizo hayo leo wakati alipotembelea kituo hicho na kujionea mwendelezo wake ambao amesema bado hauridhishi kwani wapo nje ya muda kwani kilitakiwa kukamilika desemba mwaka huu.
Pia Waziri Kalemani amepiga marufuku kwa Meneja wa Tanesco Kanda ya kaskazini,mkoa na wilaya kutokwenda likizo ya sikukuu na mwaka mpya badala yake sikukuu yao waifanyae katika eneo hilo la mradi hadi wahakikishe kazi hiyo inaridhisha katika kiwango kinachotakiwa.
Waziri alitoa siku tatu kwa Meneja mradi msimamizi wa Tanesco ,Timothy Mgaya na Mhandisi mradi msimamizi wa Tanesco ,Blandina Joachim kutoa maelezo kwa nini mradi huo umesimama na hakuna wafanyakazi na endapo hataridhishwa na maelezo hayo watatolewa kwenye kitengo hicho na kupewa watu wengine wenye uwezo wa kusimamia .
Aidha Waziri alisema kuwa,hajaridhishwa na kasi ya mradi wa kituo hicho jinsi unavyoenda kwani mradi ulitakiwa kukamilika desemba mwaka huu lakini hadi sasa hivi umekamilika kwa asilimia 46 kitendo ambacho hakiridhishi.
Naye Mhandisi mradi msimamizi kutoka Tanesco ,Blandina Joachim akijibu hoja hizo za kucheleweshwa kwa mradi alisema kuwa, changamoto kubwa ni vifaa vya mradi huo ambavyo vinatoka nje ya nchi na kuwa vimechelewa kufika kutokana na ugonjwa wa COVID 19 .
Meneja mradi Mkandarasi ,Irfan Dolgic alisema kuwa,wameshindwa kumaliza mradi huo kwa wakati kutokana na changamoto mbalimbali lakini watajitahidi kumaliza kwa wakati kulingana na maagizo ya Waziri.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment