Kampuni ya SGA Security imeibuka mshindi wa jumla kama kampuni yenye rasilimali za kutosha na ya kuaminika (Most Equipped and Reliable Security Company of the Year, 2020) katika tuzo za chaguo la wateja (Consumer Choice Award) zilizofanyika Jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
SGA Security ilikuwa inachuana na kampuni nyingine saba za ulinzi ambapo wateja walitakiwa kupiga kura kwa njia ya mtandao kwa muda wa mwezi mmoja mfulululizo kuanzia Novemba 5, 2020.
Baada ya kutangazwa washindi, walinzi wa SGA Security waliibuka kwa furaha huku wakimsindikiza Mkurugenzi wao, Eric Sambu katika jukwaa kuu kupokea tuzo hiyo.
Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo hiyo, Bw. Sambu alisema imekuja wakati muafaka ambapo SGA inaadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwake na kwamba ndio ilikuwa kampuni ya kwanza ya ulinzi kusajiliwa nchini Tanzania huku ikiitwa Group 4 Security (T) na ikawa kampuni inayoongoza kuanzia hapo hadi sasa huku ikiwa imeajiri zaidiya wafanyakazi 6000 kwa sasa.
“Tuzo hii tunawatunuku wateja wetu kwa kuwa na imani kwetu kwa huduma tunazotoa. Hii inatupa motisha kufanya kazi kwa bidii zaidi ili kuhakikisha wanaona thamani ya fedha wanazolipa,” alisema Bw. Sambu.
Aliwapongeza wafanyakazi wa SGA kwa kuifanya kampuni iwe bora zaidi kutokana na utendaji wao uliotukuka.
“Kuna makampuni zaidi ya 2000 ya ulinzi nchini Tanzania lakini kinachotutofautisha nao ni jinsi tunavyotoa huduma kwa wateja. Tuzo hii inadhihirisha kuwa tunaelewa wanachohitaji wateja na tunaelewa namna ya kuwapa huduma hizi. Tunatoa kipaumbele kwa wafanyakazi ili waendelee kutoa huduma bora na kukidhi matarajio ya wateja,” alisema.
Kwa upande wake, Meneja Masoko wa SGA, Faustina Shoo alisema kwao ni furaha kupokea tuzo hiyo hasa katika mwaka uliokuwa na changamoto nyingi kubwa ikiwa ni janga la Covid-19. “Sisi SGA tuliweka umuhimu wote kwa mteja na tuliwapa kipaumbele na kwa pamoja tuliweza kulishinda janga hili tunawashukuru kwa kweli,”alisema.
SGA Security inatoa huduma mbalimbali ikiwemo za ulinzi, alarm, huduma za fedha, ulinziwa kielektroniki, huduma ya kusafirisha mizigona huduma nyinginezo.
SGA pia inajivunia kuwa kampuni pekee yenye cheti cha ISO18788 c(Security Operations Management System). Pia ina ISO 9001: 2015 na ISO 45000:2018 (Occupation Health and Safety).
Bw. Sambu alisema kampuni hiyo pia inajivunia ushirikiano na Jeshi la Polisi hasa katika masuala ya mafunzo, udaili, na pia katika operesheni za pamoja.
Alitoa wito kwa makampuni mengine yaige mambo yanayofanywa na SGA ikiwemo kuzingatia viwango katika huduma huku pia wakikumbuka kuwajali wafanyakazi wao kwa kuwalipa vizuri na kwa wakati ili wapate ari ya kufanya kazi. “Uwekezaji katika watu ni jambo muhimu sana, mafunzo ya mara kwa mara kama inavohitajika na Jeshi la Polisi ni muhimu,” alisema huku akisisitiza kuwa wataendelea kuwekeza katika watu na teknolojia
Alisema wamepania kushinda tuzo hiyo tena mwakani huku akiwashukuru waandaaji kwa namna walivyoendesha zoezi hilo la kuwapata washindi kwa kutoa fursa kwa wateja kuchagua hivi kufanya tuzo hizi kuwa bora zaidi na za kuaminika katika ukanda huu kwani itakuwa chachu kubwa ya utoaji wa huduma zenye ubora wa juu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya SGA Security, Eric Sambu akionesha tuzo ambayo kampuni hiyo ilishinda baada ya kuibuka mshindi wa jumla kama kampuni yenye rasilimali za kutosha na ya kuaminika (Most Equipped and Reliable Security Company of the Year, 2020) katika tuzo za chaguo la wateja (Tanzania Consumer Choice Awards) zilizofanyika Jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Wafanyakazi wa SGA Security wakiungana na Mkurugenzi Mtendaji, Eric Sambu (aliyenyanyua tuzo) baada ya kampuni hiyo kuibuka mshindi wa jumla kama kampuni yenye rasilimali za kutosha na ya kuaminika (Most Equipped and Reliable Security Company of the Year, 2020) katika tuzo za chaguo la wateja (Tanzania Consumer Choice Awards) zilizofanyika Jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment