***************************************************
NA VICTOR MASANGU,PWANI
Waziri wa maji Juma Aweso ameahidi kulivalia njuga changamoto ya baadhi ya wafugaji wenye tabia ya kutitisha mifugo yao katika vyanzo mbali mbali vya maji kwani kufanya hivyo kunasababisha kuchafua maji ambayo yanatumiwa na binadamu hivyo kunaweza kuhatarisha usalama wa afya za wananchi na kuibuka kwa mlipuko wa magonjwa.
Aweso aliyasema wakati wa ziara yake ya kikazi katika wilaya mbali mbali za Mkoani Pwani kwa lengo la kuweza kuzungumza na watendaji, viongozi wa serikali, wakandarasi pamoja na kutembelea miradi mbali mbali ya maji ambayo inasimamiwa na Dawasa pamoja na Ruwasa ili kuweza kujionea shughuli zinazofanyika na kubaini changamoto zilizopo iloi kuweza kuzitafutia ufumbuzi hasa katika maeneo yaliyopo vijijini.
Pia aliongeza kwamba serikali ya wamu ya tano lengo lake kubwa ni kuhakikisha kwamba inawasaidia wananchi kuondokana na changamoto ya kutembea umbari mrefu kwa ajili ya kwenda kutafuta maji katika maeneo mengine kwa kuboresha huduma za maji pamoja na kuchimba visima.
“Serikali ya awamu ya tano nia yake kubwa ni kuboresha huduma ya maji safi na salama katika maeneo mbali mbali hususan ya vijijini, ili waweze kupata fursa ya kuweza kuchota maji kwa urahisi kutokana na huduma hiyo kuwepo karibu kwa hivyo jitihada kubwa bado zinafanyika katika sehemu mbali mbali zenye changamoto ya ukosefu wa maji,”alisema Aweso.
Pia Awezo aliongeza kuwa kwa sasa serikali imeweka mipango madhubuti ya kuongeza zaidi wataalamu wa maji ambao wataweza kusaidiana na Wizara husika kwa lengo la kuweza kusimamia miradi mbali mbali ambayo itaweza kuleta chachu zaidi na kuwasaidia wananchi kuondokana na adha ambayo wamekuwa wakikumbana nayo.
Aidha Waziri Awezo aliongeza kuwa upatikanaji wa maji safi na salama kutaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kuondokana na changamoto ya wananchi kupatwa na magonjwa mbali mbali ya mlipuko kama vile kuumwa na matumbo hasa katika maeneo ya vijijini na badaala yake serikali inajikita zaidi katika kuwapatia huduma ya maji ambayo yapo salama kwa matumizi ya binadamu.
“Wananchi kwa kweli wanapata tabu na Rais wetu mpendwa wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli ameweza kutupa dhamana kwa ajili ya kuweza kuwatumikia wananchi hivyo nitahakikisha kwamba wakandarasi ambao wamepewa kazi ya kusimamia miradi yote ya maji inatekelezeka kwa kiwango na wakati,”alibaisha Waziri Aweso.
Katika hatua nyingie Waziri aweso alibainisha kwamba endapo watalaamu wa maji na wakandarasi wakitimiza wajibu wao ipaswavyo kwa kushirikiana na Wizara basi kutaweza kuleta mabadiliko makubwa katika maendeleo ya maji na kuwakomboa wananchi kuondokana kabisa na kutembea umbari mrefu kutafuta maji na baadhi yao kuondokana na kunywa maji machafu ambayo sio salama kwa afya yao kwani yanaweza kupelekea kupata magonjwa ya milipuko.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment