Na Chalila Kibuda,Michuzi Tv
BODI ya maziwa nchini imekamata tani tatu za maziwa ya unga ya 'Cowbell' yaliyokuwa yanakaribia kuishiwa muda wa matumizi yakiwa yameongezwa muda wa matumizi zaidi.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam Kaimu Msajili wa Bodi ya Maziwa Nchini Noel Byamungu amesema walibaini kitendo hicho katika kiwanda cha Kampuni ya Hawai Limited Kilichopo Keko Chang'ombe wakiwa katika majukumu yao ya ukaguzi na usimamizi wa kuhakikisha wananchi wanapata maziwa bora.
Amesema Maziwa hayo yalitakiwa kumaliza muda wake wa matumizi Mwezi June, Agosti na Oktoba mwaka huu lakini kiwanda hicho kilifanya kitendo cha Kufunga upya maziwa hayo katika vifungashio vipya vinavyoonesha mwisho wa matumizi ya maziwa hayo kuendelea kutumika hadi Mwezi Augusti Mwaka 2022.
Amesema watendaji wamewaachia Jeshi la Polisi mkoa wa Kipolisi Temeke ambao ni Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Ahemed Suleiman Mohamed pamoja na Meneja uzalishaji Ahmed Amanzi kujibu tuhuma zinazowakabili.
Kamishina Msaidizi wa Mkoa Kipolisi Temeke Amon Kakwale amesema tayari wanawashikilia watendaji wa Kampuni hiyo.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment