DKT. FAUSTINE NDUGULILE AIPONGEZA TTCL KWA KUJIENDESHA KWA FAIDA | Tarimo Blog

 Ã         TTCL Yapata Faida ya Shilingi Bilioni 5 kwa Mwaka

à        Aitaka TTCL Iache Kufanya Biashara kwa Mazoea

à        Awataka Wawe Wabunifu, Wafanye Utafiti wa Masoko

à        Tumieni Fursa ya Shilingi Trilioni 12 Zinazopita kwenye Mitandao kwa Mwezi

 

Na Prisca Ulomi, WMTH

 Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile amelipongeza Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kwa kujiendesha kwa faida na kupunguza hasara kwa kipindi cha miaka mitano na kuacha kuacha TTCL kwa hasara

 Dkt. Ndugulile ameyasema hayo wakati akifungua kikao cha utendaji kazi wa Mameneja wa mikoa yote wa Tanzania Bara na Zanzibar wa TTCL na Menejimenti ya Shirika hilo kilichofanyika kwenye ukumbi wa Jeshi la Zimamoto, Dodoma

 Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba amemweleza Dkt. Ndugulile kuwa Shirika lake limeweza kujiendesha kwa faida kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita kuanzia mwaka 2016/2017 kwa kutengeneza faida ya shilingi bilioni tano kwa mwaka tofauti na miaka mitano iliyopita kuanzia mwaka 2016 kurudi nyuma ambapo Shirika limekuwa likijiendesha kwa hasara

 Dkt. Ndugulile ameitaka TTCL kuacha kufanya biashara kwa mazoea bali wawe wabunifu, wafanye utafiti wa masoko ili kubaini mahitaji ya wateja, kuongeza wateja na kwenda sambamba na ushindani kwa kuwa mpaka sasa TTCL ina asilimia mbili ya wateja wa simu za mkononi kwenye soko ukilinganisha na kampuni nyingine na jumla ya wateja milioni 1.3 wa simu za mkononi

 Amewaita Mameneja wa Mikoa yote ya TTCL nchi nzima ili wajadaliane na kuweka malengo yanayopimika kwa kuwa hivi sasa kiasi cha shilingi trilioni 12 zinazunguka kwenye huduma ya fedha mtandao kwa mwezi na miamala isiyozidi milioni 300 kwa mwezi zinapita mtandaoni ili TTCL itumie fursa hii kufanya biashara na kutoa gawio

 Amesisitiza kuwa kila Meneja wa Mkoa wa TTCL apewe malengo ya kuongeza wateja, kushughulikia malalamiko ya wateja kwa wakati, kutoa huduma nzuri kwa wateja na kuhakikisha kuwa ukuaji wa kuridhisha wa TTCL unaonekana

 Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Jim Yonazi amewaeleza Mameneja hao kuwa watumie mbinu za kuongeza wateja na kutengeneza mazingira ya kukubalika katika maeneo wanayotoa huduma kama ilivyo kwa waganga wa tiba za asili na wahubiri wa dini ambapo wamejenga imani na wanatoa huduma kwa wafuasi wao

 Pamoja na kikao hicho, washiriki wamepatiwa mada kuhusu Mkakati wa Kurahisisha Uongozi na Ushirikiano na Ofisi za Serikali Mikoani na Mamlaka za Serikali za Mitaa kutoka kwa Johnson Nyingi wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI na mada kuhusu utawala bora kutoka kwa Apolinari Tamayamali, Mkurugenzi wa Utawala Bora, Ofisi ya Rais – Ikulu

 

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari


Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile akisisitiza jambo kwa Mameneja wa Mikoa wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (hawapo pichani) wakati akifungua kikao cha utendaji kazi wa Shirika hilo, Dodoma.  Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Jim Yonazi na kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Waziri Kindamba.

 

Baadhi ya Mameneja wa Shirika la Mawasiliano Tanzania wakifurahia jambo wakati Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile (hayupo pichani) akifungua kikao kazi cha utendaji kazi wa Shirika hilo, Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi akizungumza kumkaribisha Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Faustine Ndugulile (aliyeketi katikati) kabla ya kufungua kikao cha utendaji kazi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania, Dodoma. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Waziri Kindamba

 

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania, Waziri Kindamba akifafanua jambo kwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile (aliyeketi katikati) kwenye kikao cha utendaji kazi wa Shirika hilo kilichowakutanisha Mameneja wa Mikoa wote wa Shirika hilo (hawapo pichani), Dodoma. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Jim Yonazi

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile (aliyeketi katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Menejimenti ya Shirika la Mawasiliano Tanzania baada ya kufungua kikao cha utendaji kazi wa Shirika hilo, Dodoma. Wa kwanza kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Jim Yonazi na wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Waziri Kindamba

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile (wa pili kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Naibu Katibu wa Wizara hiyo, Dkt. Jim Yonazi (wa pili kulia) baada ya kufungua kikao cha utendaji kazi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania, Dodoma. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Waziri Kindamba na wengine wanatoka Wizara hiyo, TAMISEMI, Ofisi ya Rais – Ikulu na Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Hassan Mwang’ombe (wa tatu kulia aliyesimama)


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2