Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa akionyesha aina ya magari wanayoshikilia na mahali yalikopatikana ili kuwasaidia wenye mali zao kuzitambua.
Na Amiri Kilagalila, Njombe
WATUHUMIWA 5 wanashikiliwa na jeshi la polisi Mkoa wa Njombe kwa tuhuma za kuhusika na wizi wa magari 6 yaliyopatikana mikoa tofauti yanayosadikika yametokana na ujambazi.
Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa amesema wanashikilia gari 6 yaliyoibwa katika maeneo tofauti huku watuhumiwa 5 wakiendelee kuwahoji juu ya kuhusika na tuhuma za wizi huo.
“Tulikuwa tunatafuta gari moja matokeo yake tumeweza kukamata gari zingine 6 ambazo zinahusishwa na kuibwa maeneo mbali mbali katika nchi yetu.”Alisema Kamanda Issa.
Kamanda aewataja watuhumiwa hao kuwa ni pamoja na
“Kuna mshtakiwa maarufu Endrick Husein jina maarufu (Kimya kimya) huyu ni mkazi wa Dar es salaam, Sudy Mwinyi mkazi wa Uyole Mbeya, Method Mkongwa mkazi wa Njombe, Iman Phidelis mkazi wa Moshi fundi magari pamoja na Timoth Nehemia mkazi wa Mufindi hawa wanashirikina kuiba magari na kuyapokea.”alisema Hamis Issa.
Amesema gari wanazoshikiria ni pamoja na aina ya Noah rangi ya silver iliyoibwa mkoani Mbeya,Gari aina ya Spacio iliyotoka Silali mkoani Mara,Rava 4 iliyokamatwa mkoani Singida,Carina iliyopatikna mjini Njombe.
Amewataka watanzania waliopotelewa na gari hizo kufika mkoani Njombe na vielelezo ili waweze kutambua gari zao kwa kuwa kwa sasa zipo mikononi mwa polisi.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment