Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.
Angeline Mabula na Mkuu wa wilaya ya Mvomero Albinus Mugonya
wakiangalia sehemu ya maendeleo ya ujenzi wa Ofisi ya Wilaya ya Wakala
wa Huduma za Misitu (TFS) iliyopo Mvomero mkoa wa Morogoro wakati wa
ziara ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi tarehe 30 Desemba
2020.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt
Angeline Mabula na Mkuu wa wilaya ya Mvomero Albinus Mugonya
wakiangalia sehemu ya maendeleo ya ujenzi wa Ofisi ya Wilaya ya Wakala
wa Huduma za Misitu (TFS) iliyopo Mvomero mkoa wa Morogoro wakati wa
ziara ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi tarehe 30 Desemba
2020.
Naibu Waziri wa Ardhi Dkt Angeline Mabula akizungumza na
wananchi wa Yesper, Lukobe na Kiegeya mkoani Morogoro wakati wa zoezi
la kugawa Hati ya Ardhi wakati wa ziara ya kukagua utendaji kazi wa
sekta ya ardhi katika mkoa wa Morogoro tarehe 30 Desemba 2020.
sehemu ya wananchi wa Maeneo ya Yesper, Lukobe na Kiegeya
katika mkoa wa Morogoro wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ardhi Dkt
Angeline Mabula wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa sekta
ya ardhi katika mkoa wa Morogoro tarehe 30 Desemba 2020.
Naibu Waziri wa Ardhi Dkt Angeline Mabula akimkabidhi Hati ya Ardhi
mkazi wa Kiegeya mkoani Morogoro Annet Andrew wakati wa kugawa Hati
kwa wananchi wa Yesper, Lukobe na Kiegeya wakati wa ziara ya kukagua
utendaji kazi wa sekta ya ardhi katika mkoa wa Morogoro tarehe 30
Desemba 2020.
Na Munir Shemweta, MOROGORO
NAIBU Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline
Mabula amebaini ubadhilifu wa zaidi ya Bilioni 2 uliofanywa na
Wakufunzi wa Chuo Cha Ardhi Morogoro (ARIMO) na kumuelekeza Mkuu wa
Chuo Huruma Lugala kumsimamisha kazi mara moja Mkuu wa Utawala wa
Chuo Michael Lori kwa tuhuma ya kushirikiana na wakufunzi wawili wa
chuo hicho waliofanya ubadhilifu katika zoezi la urasimishaji.
Dkt Mabula alitoa maelekezo hayo tarehe 30 Desemba 2020 mkoani
Morogoro wakati akizungumza na watendaji wa sekta ya ardhi pamoja na
uongozi wa mkoa wa Morogoro akiwa katika ziara yake ya siku moja
kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi pamoja na miradi
inayotekelezwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
Alisema, Wizara yake ilifikiri kushirikisha makampuni binafsi katika
zoezi la urasimishaji ingerahisisha kazi ya kupima na kumilikisha
wananchi maeneo yao lakini matokeo yake baadhi ya makampuni na watu
wachache wametumia nafasi hiyo kufanya ulaghai wa kuchukua fedha za
wananchi bila kukamilisha kazi ya urasimishaji.
Kwa mujibu wa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
Mkuu wa Utawala katika Chuo cha Ardhi Morogoro ameonekana kushirikiana
na watuhumiwa kwa namna moja ama nyingine na uamuzi wa kumsimamisha ni
kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili.
Awali Dkt Mabula alielezwa na Mkuu wa Chuo cha Ardhi Morogoro Huruma
Lugala kuwa wakati uongozi wa chuo hicho ukifanya jitihada za
kukiboresha chuo ikiwemo kudhibiti hujuma mbalimbali ilibainia baadhi
ya Wakufunzi wake kujihusisha na kazi ya urasimishaji katika maeneo
mbalimbali kwa kutumia jina la chuo kujipatia fedha.
Alisema, chuo chake baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi na
kubainia udanganyifu kwa baadhi ya watumishi wake kiliamua
kuwasimamisha Wakufunzi wawili kupisha uchunguzi na kuwataja watumishi
hao kuwa ni Adolf Milungala anayetuhumiwa kujipatia shilingi Bilioni
1.9 na Hamis Abdalah Kindemile milioni 275 fedha zilizokuwa malipo ya
urasimishaji katika mitaa 43 Morogoro.
Hata hivyo, Mkuu huyo wa Chuo cha ARIMO alisema wakati uchunguzi
ukiendelea dhidi ya watuhumiwa, Mkuu wa Utawala Lori amekuwa
akishirikiana na watuhumiwa kukwamisha uchunguzi na hata pale
alipotakiwa kujieleza kwa barua alijibu kwa dharau na kuongeza kuwa
hata alipoitwa na tume ya uchunguzi aligoma kwa kisingizo cha ugonjwa.
Naibu Waziri Mabula aliupongeza uongozi wa Chuo cha ARIMO kwa hatua
ilizochukua za kuwasimamisha watuhumiwa kupisha uchunguzi na
kusisitiza kuwa Wizara yake imeanza kuchukua hatua kwa makampuni yote
yaliyoshindwa kukamilisha kazi za urasimishaji.
‘’ Kufuatia tukio hili halmashauri inatakiwa kuchukua hatua za
kukamilisha upimaji katika maeneo ambayo watuhumiwa walichukua fedha
na nimekiagiza Chuo cha Ardhi Morogoro kuhakikisha na kinafanya
upimaji katika maeneo hayo’’ alisema Dkt Mabula
Kwa mujibu wa Dkt Mabula, lengo la Wizara ya Ardhi ni kwamba mwananchi
aliyetoa pesa apimiwe na apate haki yake ya msingi ya kupatiwa hati
na kusisitiza kuwa hilo ni onyo kwa makapuni yote yasiyotekeleza
kazi kuchukuliwa hatua na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Katika hatua nyingine Naibu Waziri wa Ardhi Dkt Mbaula alionesha
kutoridhishwa na kasi ya ukusanyaji maduhuli ya serikali katika mkoa
wa Morogoro aliyoyaeleza kuwa hadi kufikia Desemba 2020 kiasi cha
bilioni 2.3 pekee kati ya bilioni 11 ndicho kilichokusanywa ikiwa ni
sawa na asilimia 18.
Pia alisema mkoa wa Morogoro unadai takriban Trilioni 1.06 kutoka kwa
wamiliki wa ardhi wasiolipa kodi ya pango la ardhi na kubanisha kuwa
watendaji wa sekta hiyo wamekuwa hawaoneshi juhudi zozote za kudai
fedha hizo wakati wakijua kuna madeni makubwa.
Naibu Waziri wa Ardhi aliongeza kwa kusema kuwa, Wizara yake kwa sasa
itakuwa ikiwapima wakuu wa idara za ardhi kwenye halamashauri na
Maafisa Ardhi Wateule kwa vigezo vya utendahji ikiwemo makusanyo ya
kodi na kusisitiza watakaoshindwa wataondolewa katika nafasi hizo.
Aidha, Dkt Mabula katika ziara yake mkoani Morogoro alikagua pia
ujenzi wa mradi wa Ofisi ya Wilaya ya Wakala wa Misitu Tanzania (TFS)
iliyopo Mvomero unaojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).Pamoja
na Naibu Waziri wa Ardhi kuonesha kuridhishwa na ujenzi wa miradi
inayojengwa na NHC katika maeneo mbalimbali alilitaka Shirika hilo
kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa kwa ubora na kwa gharama nafuu.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment