MANISPAA YA ILALA KUFUNGUA KIWANDA CHA NYAMA CHA WANAWAKE | Tarimo Blog


NA HERI SHAABAN

HALMASHAURI ya Manispaa Ilala jijini Dar es salaam inatarajia kufungua Kiwanda cha nyama kitakachoongozwa  na Wanawake wa Ilala.

Mikakati ya kufungua kiwanda hicho yamekamilika kitafunguliwa hivi karibuni ofisi zake zitakuwa Vingunguti Jimbo la Segerea .

Akizungumza katika tathimini ya utoaji mikopo ya asilimia kumi ya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu ambayo inatolewa ngazi ya Halmashauri, Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Jumanne Shauri amesema amefarijika na Vikundi vya wanawake waliochukua mikopo ya Serikali wamekuwa waminifu katika urejeshaji hivyo wanawamini kusimamia kiwanda hicho cha nyama.

"Tunaunga mkono juhudi za Rais wetu za John Magufuli Tanzania ya uchumi wa viwanda wilaya Ilala iwe na viwanda vya kutosha wanawake wetu wajikwamue kiuchumi "amesema.

Mkurugenzi Shauri alisema mwaka huu katika Jimbo la Segerea wanatoa Bilioni 4 ,amewataka wasiorejesha warejeshe kwa wakati kabla kuchukuliwa hatua za kisheria hasa makundi ya vijana wengi wasumbufu ndio maana kiwanda tunawakabidhi wanawake.

Kwa upande wake Ofisa Maendeleo wa Manispaa ya Ilala Fransica Makoye amesema dhumuni la kufanya tathimini ya mikopo kuongeza hamasa kwa vikundi vya mikopo wajue nini kinafanyika jimbo la Segerea maonyesho hayo ya tathimini watafanya kwa mwaka mara mbili

Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya Ilala Arch, Ng'wilabuzu Ludigija  alisema mikopo hiyo mizuri aina riba pongezi kwa Mkurugenzi wa Ilala na Ofisa Maendeleo wa Manispaa ya Ilala kwa kazi nzuri wanayosimamia .

Ludigija amesema wanaunga mkono juhudi za Rais John Magufuli kila mtu aweze kujishughulisha na kufanya kazi aweze kujipatia kipato cha halali .

Ludigija alitoa tuzo kwa vikundi vilivyorejesha kwa wakati, vya Kata ya Liwiti, Kinyerezi ikiwemo vikundi 30 walioewa vyeti vya kuvitambua.

Amewataka watumie fursa vizuri ya mikopo ya Manispaa ya Ilala warejeshe kwa wakati pesa ya serikali lazima irejeshwe.

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Segerea  Bonnah  Kamoli ameishukuru serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na  Dk. Magufuli kwa kuviwezesha vikundi vya ujasiriamali vya wanawake, vijana na wenye ulemavu jimboni kwake.

 Bonnah alieleza kuwa kwa kiasi kikubwa wajasiriamali wa jimbo la Segerea wamenufaishwa na uwezeshwaji unaofanywa na serikali Kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Arch Ng'wilabuzu Ludigija akipanda bodaboda  za mikopo katika maonyesho ya Tathimini ya mikopo Jimbo LA segerea yakioandaliwa na Manispaa ya Ilala January 13/2021 (PICHA NA HERI SHAABAN)
Afisa Maendeleo Kata ya Buguruni akipewa cheti cha shukrani Mkuu wa Wilaya ya Ilala Arch Ng'wilabuzu Ludigija January 13/2021 vyeti hivyo vimetolewa na Manispaa ya Ilala ,Afisa Maendeleo huyu wa Buguruni alifanya kazi zake kwa Weledi (Kulia )Mbunge wa Segerea Bonah Ladslaus Kamoli
Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto akiangalia bidhaa za wajasiriamali wakati wa Tathimini ya mikopo Jimbo LA Segerea (kutoka kulia )Afisa Maendeleo Ilala Fransica Makoye na Mkurugenzi wa Manispaa Jumanne Shauri.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Arch Ng'wilabuzu Ludigija akiwa na Mbunge wa Segerea Bobah Ladslaus Kamoli katika Tathimini  ya mikopo  Jimbo LA segerea yakioandaliwa na Manispaa ya Ilala.

Meya wa Halmashauri ya Ilala Omary Kumbilamoto akiongea na Mbunge wa Jimbo LA Segerea Bonah Ladslaus Kamoli wakati wa Tathimini ya mikopo Jimbo segerea (kulia)Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Jumanne Shauri (PICHA na HERI SHAABAN)



Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2